Header Ads Widget

MUSOMA VETERAN MABINGWA WA BONANZA LA PASAKA 2025 SIMIYU

 


Na -Shomari Binda-Matukio Daima

TIMU ya Musoma Veteran imefanikiwa kutwaa ubingwa wa bonanza la Pasaka kwa timu za Veteran lililofanyika mkoani Simiyu.

Bonanza hilo lililofanyika kwa siku 2 aprili 18 na 19 limefanyika kwenye uwanja Halmashauri ya Bariadi na kushirikisha timu 7 kutoka Kanda ya Ziwa.

Musoma Veteran imetwaa ubingwa huo kwa kuifunga timu timu ya Biashara United Veteran ya mjini Musoma mabao 2-0


Akizungumza mara baada ya kuhitimishwa kwa bonanza hilo kocha wa timu ya Musoma  Veteran Ramadhan Magoye amesema siri ya kufanya vizuri ni mazoezi na kujitunza kwa wachezaji.


Amesema licha ya kutwaa ubingwa huo bonanza lilikuwa gumu na timu zote shiriki zilikuwa zimejipanga vizuri kushiriki bonanza hilo.


Magoye amesema katika mchezo wa fainali dhidi ya Biashara United Veteran ulikuwa mgumu zaidi kutokana na kufahamiana zaidi na wapinzani wao.



Musoma Veteran imetokea kundi A ikiwa na timu za Kishapu Veteran na Simiyu Veteran na iliiondosha timu ya Bunda Veteran kwenye mchezo wa nusu fainali.


Kwa upande wa Biashara United Veteran wametokea kundi B ikiwa na timu ya Shinyanga Town Veteran,Bunda Veteran na Misungwi Veteran na kuitoa timu ya Simiyu Veteran kwenye mchezo wa nusu fainali

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI