Header Ads Widget

POLISI YAKAMATA GARI YENYE SHEHENA ZA DAWA ZINAZODHANIWA ZA KULEVYA IKIINGIA TOKA MALAWI.

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kupambana na kudhibiti dawa za kulevya Aprili 19, 2025 huko Wilayani Rungwe limefanyika kukamata Gari lenye namba za usajili T. 833 EDN aina ya Mitsubishi Canter likiwa limebeba shehena ya dawa zinazodhaniwa za  kulevya aina ya Bhangi.

Akizungumzia hatua ya ukamatwaji wa dawa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga, amesema kuwa Gari imeingia nchini ikitokea nchi jirani ya Malawi ikiwa na jumla ya vifurushi 67 vyenye dawa za kulevya aina ya bhangi yenye uzito wa kilogram 1500.

Kamanda Kuzaga amewataka wananchi kujiepusha na biashara haramu ya dawa za kulevya kwani Jeshi la Polisi Mkoani humo lipo imara kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI