Na Shomari Binda-Musoma
JUMLA ya wanawake 30 wamependekezwa kuwania tuzo kwenye vipengele 8 kwenye usiku wa mwanamke gara mkoa wa Mara aprili 27,2025
Akizungumza na Matukio Daima kuelekea tukio hilo,Anifa Majura maarufu kama "mama Fugo"ambaye ni mratibu amesema zoezi la upigaji kura limeanza ili kuwapata wanawake vinara.
Amesema huu ni msimu wa pili na mwaka huu tukio hilo limeonekana kupokelewa vizuri tangu kuanza kwa maandalizi yake.
Mratibu huyo amesema kwa sasa zoezi la kuwapigia kura washiriki linaendelea vizuri pamoja na maandalizi ya yote ya siku hiyo.
Ametaja vipengele vinavyowaniwa ni pamoja na mwanamke bora mbunifu ushonaji nguo,kikundi bora cha wanawake,mwanamke mfanyabiashara,upishi na upambaji wa keki,saloon bora ya kike,sekta ya habariushereheshaji matukio na sekta ya uvuvi,ufugaji na kilimo.
Amesema washiriki wanapaswa kuendelea kuomba kura kwa utaratibu uliowekwa kwa namba zinazotumika na kuwahakikishia mshindi atapatikana kupitia wingi wa kura na si vinginevyo.
" Tunashukuru Mungu maandalizi ya tukio letu linalokwenda kufanyika aprili 27 yanakwenda vizuri kwa namna lilivyopangiliwa.
" Burudani zipo nyingi zikiongozwa na msanii mkubwa Christian Bella likinogeshwa na Mc Mziwanda hivyo mambo yatakuwa moto watu wajiandae kwa tukio la tofauti Musoma",amesema.
Mratibu huyo amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini tukio hilo ili kuwashika mkono wanawake lengo likiwa kuwainua kwenye shughuli zao za kiuchumi.
0 Comments