Na Matukio Daima Media
IDADI ya watu 7 wamepoteza maisha na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari la kubebea wagonjwa (ambulance) na guta iliyokuwa imebeba watu 22 Mjini Mafinga barabara ya kwenda Luganga karibu na ofisi za Halmashauri ya Mji wa Mafinga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa alipofika katika Hosipitali ya Mji wa Mafinga inaeleza kuwa watu hao walikuwa wanakwenda shamba kwa kutumia usafiri ambao ni hatarishi kwao na hapa anatoa wito kwa wananchi
Akithibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi wa ajali hiyo Mganga Mafawidhi wa Hosipitali ya Mji wa Mafinga Dkt.Victor Msafiri amesema majira ya saa kumi na mbili asubuhi wamepokea majeruhi 15 na miili 7 huku akieleza hali za majeruhi hao
0 Comments