Header Ads Widget

VIJANA MKOANI MTWARA WAOMBWA KUCHANGAMKIA FURUSA YA AJIRA.



Na Matukio Daima Media,Mtwara

Ajira  takribani 550 zinatarajiwa kutolewa kwa vijana mkoani Mtwara katika  kada tofauti tofauti hivyo wameombwa  kuchangamkia  fursa hizo.


Vijanana wameombwa kuchangamkia fursa hizo ili ziwasaidie kujikwamua kiuchumi hayo yamesemwa  na mkurugenzi  wa kampuni ya ulinzi ya Asgardsecurity.


Mkurungnzi wa kampuni hiyo ya ulinzi  Samweli Magita amesema wanawahitaji vijana katika kada ya ulinzi,wasimamizi wa ofisi,wauguzi ,madereva,watunza taarifa na wengine ni wataalamu wa zima moto na watembea na mbwa muombaji awe na barua ya maombi,barua ya serikali ya mtaa,namba ya nida,picha mbili(pasport) na wazamini wawili wenye barua ya mwenyekiti wa mtaa.


"Tunahitaji vijana 550 hamsini katika nyanja tofauti tofauti wakishapatikana tutawaandaa kwakuwapa mafunzo kisha wataanza kazi.Kwawale watakaotoka nje ya Mtwara tumeandaa maeneo la makazi pia tutatoa gharama za usafiri na chakula hadi tutakapoanza kulipa mishahara"amesema Samweli.


Mkurugenzi huyo wa kampuni ya ulinzi ya Asgardsecurity  amezitaja nafasi hizo kuwani,wafanyakazi wa majumbani,walizi wakawaida 300 na walinzi wa kutumia silaa 50,watunza taarifa10 ,madereva 20,wauguzi5 na wasimamizi wa ofisi 5 nafasi nyingine ni wataalamu wa uzimaji moto  20.


"Waombaji wana weza kutumia barua pepe kwawale waliopo nje ya Mtwara ambayo ni info@asgardsecurity.co.tz ama namba za simu 0742373932,0745146249,0713482318 ama anaweza kutumia namba 0658385515,0655957525 na 0715397813 na kwaupande wa Mtwara mjini wanapatikana Rahaleo karibu na banki ya DTB"


"Maombi yatumwe kuanzia leo tarehe  aprili 17  na mwisho ni tarehe mai 17 ndiyo mwisho lakini kwa waliopo Dar es saalamu wanaweza kupeleka makao makuu  ya kampuni yapo Mwembeni Kinyerezi  kituo cha mwembeni kwa upande wa Mwanza ofusi ipo idara ya Madini zamani nyumba namba 3 hizo ndizo sehemu maombi yetu yanapokelewa"amesema Samwel.

Kwaupande wake Afisa rasilimali watu wa kampuni hiyo ya Asgardsecurity Company Mfumbwa Mzige.


"Vijana wasiogope kuomba waombe unaweza usiwe na kigezo cha elimu lakini muonekano wako ukakupatia nafasi  kikubwa ukiwa unaomba ufuate taratibu zilizo wekwa na barua utakayo andika iseme unaomba kazi gani na uwe na barua ya maombi na wazamini wawili  waandike barua nao wawe na barua kutoka serikali ya mtaa" amesema Mzige.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI