Header Ads Widget

MAHAKAMA KENYA YAAGIZA VITUO VYA UTANGAZAJI VILIVYOZUIWA KURUSHA MUBASHARA MAANDAMANO KUFANYA KAZI


Mahakama Kuu imetangaza kusitisha agizo la Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) la kupiga marufuku vituo vyote vya runinga na redio kurusha matangazo ya moja kwa moja ya maandamano, na kwamba kituo chochote kilichozimwa kutokana na agizo hilo kirejeshwe hewani mara moja


Jaji Chacha Mwita, ameagiza vituo vya NTV, KTN na K24 kurejeshwa hewani kutokana na ombi lililowasilishwa na Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK) na Chama cha Wahariri wa Kenya (KEG) kuhusu hatua iliyochukuliwa na Serikali


Matangazo ya vituo hivyo yalizimwa wakati kukiwa na maandamano makubwa ya kitaifa dhidi ya Serikali, kuadhimisha Mwaka mmoja tangu maandamano ya Juni 25, 2024 ya Vijana ya kupinga muswada wa fedha, yaliyogharimu maisha ya takriban Watu 60



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI