Header Ads Widget

MBUNGE MUHONGO ATAJA AJIRA ZA NJE YA NCHI KAMA FURSA NYINGINE KUINUA UCHUMI

 


Na Shomari Binda-Musoma 

MBUNGE wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo ametaja ajira mpya za nje ya nchi kama fursa nyingine ya kuinua uchumi.


Hayo ameyasema leo aprili 14 bungeni jijini Dodoma wakati akitoa mchango wake alipokuwa akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Kikao cha 5 cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12.



Amesema ajira za nje ya nchi  ni bidhaa mpya duniani ambayo ambayo mwaka jana 2024 ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 905.


Muhongo amesema sifa ya ajira ni elimu na mafunzo na ajira kubwa inatokana na sekta binaafsi na sio lazima kuajiliwa Tanzania bali mataifa ya Ulaya,Marekani na mengineyo.


Mbunge huyo ameyataja meneo manne yakiwemo ya afya na teknolojia ambayo yana nafasi kubwa ya ajira nje ya nchi kwenye sekta binafsi.


Amesema umuhimu wa kazi za nje ni vijana kupata ajira na taifa kupata fedha za nje ambazo zitaendelea kuongeza uchumi wa taifa na vijana wenyewe.


Awali akitoa mchango wake amezungumzia Sera ya Taifa ya Maafa na kudai inahitaji marekebisho makubwa ili iendane na hali halisi iliyopo hivi sasa.

-

“Sera yetu tuliyonayo hivi sasa haiendani na hali halisi kwasababu maafa yamekuwa ni mengi na ya aina tofauti tofauti kwa mfano sasa tuna maafa yanayotokana na mabadiliko tabianchi hayo ni kama ukame, mafuriko, dhoruba huko ziwani na mengine.

-

"Sababu ya pili ya kufanyika kwa maboresho ya sera hiyo ni ongezeko la idadi ya watu lililopo hivi sasa na maafa yakitokea tunakosa nafasi nzuri ya kukabiliana nayo",amesema.


Kupitia mchango huo a.metoa pole kwa kaya 84 zilizopaya maafa Musoma vijijinikutokana na mvua pamoja na kaya zaidi ya mia 30 manispaa ya Musoma na kuomba wabunge waipitishe bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu ili iweze kutekeleza majukumu yake

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI