Na Hamida Rmadhan,Matukio Daima App Dodoma
KATIKA kuhakikisha unakuza na kudumishwa Utamaduni wa Kitanzania katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita, Wizara imeratibu jumla ya Matamasha matatu (3) ya Kitaifa ya Utamaduni nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akieleza mafanikio ya awamu ya Sita ya Wizara hiyo ,Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Profesa Palamgama Kabudi amesema Tamasha la Kwanza la Utamaduni wa Mtanzania lilifanyika mwezi Juni, 2022, jijini Dodoma, Tamasha la Pili lilifanyika mwezi Agosti, 2023, mkoani Njombe, na Tamasha la Tatu lilifanyika mwezi Septemba, 2024, mkoani Ruvuma.
Amesema Matamasha hayo yamelenga kuonesha na kudumisha tamaduni za makabila ya Tanzania kwa maonesho ya ngoma, sanaa, na michezo ya asili, na pia yamekuwa jukwaa la kuhamasisha wananchi kushiriki katika kuenzi na kudumisha urithi wa utamaduni wa Kitanzania.
Mafanikio ya Siku ya Maadhimisho ya Kiswahili
Amesema Katika kipindi kifupi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, Serikali imefanikiwa kutambua na kuenzi Kiswahili kama lugha muhimu kimataifa.
" Hii ni baada ya tarehe 7 Julai kutambuliwa rasmi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kama Siku ya Kiswahili Duniani," Amesema
Na kuongeza "Uamuzi huu ulifanyika mnamo tarehe 1 Julai, 2024, katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani ambapo Mafanikio haya yanadhihirisha uongozi thabiti wa Serikali ya Awamu ya Sita katika kukuza na kutangaza Kiswahili katika jukwaa la kimataifa, " Amesema
Pia Serikali kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) imeratibu Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili, lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Havana, nchini Kuba, kuanzia tarehe 07 hadi 10 Novemba 2024.
Kongamano hilo limekuwa hatua muhimu katika kuimarisha Kiswahili kama lugha yenye umaarufu na umuhimu katika majukwaa ya kimataifa, na pia limeongeza utambulisho wa Tanzania duniani kote.
"Pamoja na kongamano hili, BAKITA lilizindua Kamusi ya Kiswahili - Kihispaniola, hatua ambayo imeendelea kukuza na kueneza Kiswahili," Amesema.
Na kuongeza"Kongamano hilo lilihusisha washiriki takribani 600, likiongozwa na kaulimbiu isemayo: Ustawi wa Kiswahili Duniani: Tulikotoka, Tulipo na Tunakokwenda, " Amesema
Aidha Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi cha miaka minne, imefanikiwa kufungua vituo 19 vya kufundisha Kiswahili kupitia balozi za Tanzania katika nchi za Uholanzi, Abu Dhabi, Italia, Zimbabwe, Nigeria, Uswisi, Ufaransa, na Uturuki.
" Hii inafanya kuwa na jumla ya vituo 19 vya kufundisha Kiswahili nje ya Tanzania na hatua hii ni muhimu katika kukuza na kueneza Kiswahili duniani kote, na inachangia katika kuongeza umaarufu wa lugha hii katika maeneo mbalimbali ya kimataifa, Ambapo kwa sasa ni miongoni mwa lugha 7 kubwa zaidi Duniani yenye takribani wazungumzaji takribani millioni 500," Ameleza
SEKTA YA MAENDELEO YA SANAA
Ugawaji wa Mirabaha kwa Wasanii
Kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya Sita, Serikali kupitia COSOTA imefanikiwa kusimamia ukusanyaji wa mirabaha na kugawa gawio kwa wasanii nchini. Ambapo, katika kipindi hicho, jumla ya Shilingi 1,428,105,240.00 zimekusanywa kutokana na Tozo ya Hakimiliki (Copyright Levy), ambapo asilimia 60 ya fedha hizo, zitagawiwa kwa wasanii kama gawio la mirabaha mwezi Mei, 2025.
Uhuishaji na Uendelezaji wa Tamasha la Serengeti Music Festival
Serikali imefanikiwa kuhuisha na kuimarisha Tamasha la Serengeti Music Festival ambalo kwa sasa linajulikana kama Samia Serengeti Music Festival, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais ya kuibua vipaji vya vijana, kukuza ajira na kutangaza utamaduni wa Taifa letu.
Kwa mara ya kwanza, tamasha hili liliandaliwa mwaka wa fedha 2020/21 katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Tangu wakati huo, limeendelea kukua kwa kasi na kufanyika kwa mafanikio katika maeneo mbalimbali nchini, huku likiwa sehemu ya mkakati wa kuunganisha wasanii wa ndani na masoko ya kitaifa na kimataifa.
SEKTA YA HABARI
Katika kuhakikisha Watanzania wanaendelea kupata taarifa kuhusu utekelezaji wa Serikali yao, Msemaji Mkuu wa Serikali amefanya mikutano 43 kuelezea utekelezaji wa Serikali na kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali na pia kufanya ziara katika vyombo vya habari kuelezea masuala mbalimbali ya nchi.
Aidha, Wizara kupitia Idara hii imeendelea kuzalisha maudhui mbalimbali kuhusu utekelezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita na kuyasambaza kwa wananchi kupitia Televisheni, Radio, Magazeti na mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuhakikisha Watanzania wanapata taarifa kuhusu utekelezaji wa Serikali yao;
Amesema Iamdara ya Habari-MAELEZO imeimarishwa kwa kununuliwa vitendea kazi vikiwemo magari na vifaa vya kurushia matangazo mbashara na kuvilisha matangazo hayo vyombo vingine vya habari vya Televusheni na Televisheni Mtandao hata katika katika mkutano huu, MAELEZO ndio wanafanya uzalishaji wa maudhui mbashara na kuvilisha vyombo vyombo vingine vya habari;
Amesema Wizara kupoitia Idara ya Habari MAELEZO imeendelea kuratibu Waandishi wa Habari na masuala ya mawasiliano wakati wa majanga ili kuhakikisha Watanzania wanapata taarifa sahihi.
"Kazi hii imefanyika kwa mafanikio makubwa wakati nchi yetu ilipapata janga la maporomoko ya tope na mawe kule Hanang mkoani Manyara pamoja na ajali ya kuanguka kwa ghorofa eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam mwaka 2024," Amesema.
Aidha, Wizara imeendelea kutekeleza jukumu la uratibu wa Waandishi wa Habari katika shughuli za kitaifa pamoja na ziara za viongozi wakuu wa ndani na wale wa nchi zingine wanaofanya ziara nchini kwetu pamoja na uratibu wa Waandishi wa Habari katika mikutano mikubwa ya kimataifa inayofanyika nchni;
Mwisho
0 Comments