Header Ads Widget

MWENYEKITI UVCCM TAIFA AWATAKA VIJANA WASITUMIKE KUVURUGA AMANI YA NCHI

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM Taifa Mohamed Ali Kawaida amewaonya vijana kujiepusha kutumika kuvuruga amani iliyopo kwani machafuko mengi yanayoripotiwa kwenye mataifa mengine vijana ndio wanaotumika.



Kawaida ametoa onyo Hilo akiwa Mjini Njombe katika mwendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani hapa na kwamba vijana wanapaswa kujiepusha kutumika kuvuruga amani hasa kuelekea katika uchaguzi mkuu Ujao kwani Kuna mataifa jirani yapo kwenye vita kubwa inayochagizwa na vijana.


Erick Ngole ni  Mwenyekiti wa vijana UVCCM wilaya ya Njombe ambaye amesema vijana kwa sasa hawako Tayari kuona wanatumika vibaya kwa maslahi yao binafsi na kwamba safari hii watapambana nao.


Katibu wa Itikadi uenezi na mafunzo CCM mkoa wa Njombe Josaya Luoga amekiri kuwa Hali ya Siasa ni shwari na wamejipanga kushinda kata zote na majimbo yote katika uchaguzi Mkuu ujao.



Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga amemuomba Mwenyekiti wa vijana kwenda kumpelekea salamu Rais wa Samia kuwa Wanatarajia kuanza kwa miradi mikubwa ya Madini ya Chuma na Makaa ya Mawe huko Ludewa kwani wananchi Wana hamu kubwa ya kuona utekelezaji baada ya zoezi la ulipwaji fidia Kufanyika.


Kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Njombe,Mkuu wa wilaya ya Njombe Juma Sweda amesema Serikali itaendelea kuwashika mkono vijana kwa kuwapa mikopo isiyo na riba ili waweze kujikwamua kiuchumi huku Mwenyekiti wa Vijana mkoa Samwel Mgaya amesema Zaidi ya shilingi bilioni 2 zimeshatolewa kwa vijana.


Pia Mgaya amesema vijana wamechoka kubeba mabegi ya wagombea na hivyo wanataka kila nafasi vijana washiriki huku wakifanya Siasa safi.


Hata hivyo Ivan Moshi Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa na Mwenyekiti wa vijana mkoa wa Kilimanjaro amesema vijana wanapaswa kutekeleza majukumu yao wakati wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na Kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.


Zainab Kibiki,Benedict Masasi na Benedict Mgaya ni baadhi ya vijana ambao wamekiri kupokea maelekezo ya Mwenyekiti wao na kwamba hawako Tayari kutumika kuvuruga amani ya nchi Wala kutumika kisiasa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI