Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI ATAKA MASHOGA WATENGWE KWENYE JAMII

 


Naibu Waziri wa Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum, MaryPrisca Mahundi  akizungumza katika kongamano la kupinga ukatili Manispaa ya Kigoma Ujiji

Na Fadhili Abdallah ,Kigoma

Naibu Waziri wa Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum, MaryPrisca Mahundi ameitaka jamii kuwatenga wanaume wanaojishughulisha na vitendo vya ushoga,ubakaji na ulawiti kwa kuangiliwa au kushiriki kuingilia wengine kinyume na maumbile kwani watu wanaofanya vitendo hivyo wanaishi kwenye jamii mtaani.


Naibu Waziri Mahundi alisema hayo wakati wa kangamano la wadau wa kupinga ukatili mkoani Kigoma akijibu tuhuma na malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na wadau wa kupinga ukatili wakiitaka serikali kuchukua hatua kwani mambo hayo yanayonekana kama yanafumbiwa macho na serikali na ndiyo maana vitendo hivyo vinaendelea.


Akijibu tuhuma na malalamiko hayo Naibu Waziri Mahundi alisema kuwa serikali imeweka sheria kali na hatua zimekuwa zikichukuliwa kila taarifa inapotolewa kuwepo kwa vitendo hivyo na kubainisha kwamba jamii ndiyo yenyewe jukumu la kutoa taarifa kuhusu uwepo wa watu wanaofanya vitendo hivyo lakini pia kubeba jukumu kubwa la kukemea kwani wengi wa watu hao wanaishi na ndugu na jamaa zao ambao wanaona mambo hayo bila kuchukua hatua.

Akizungumza katika kongamano hilo Meya   wa Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma, Mussa Maulid ameitaka serikali kusimamia kwa karibu makosa ya ushoga ili watu wanaohusika na masuala hayo wapewe  adhabu kali  ili kuinusuru jamii na vitendo vya mmomonyoko wa maadili vinavyotokana na ushoga, ulawiti na ubakaji.

Maulid alitoa kauli hiyo mbele ya ambapo kiongozi huyo alisema kuwa vitendo vya ushoga vimevuruga sifa na maadili ya mji mkongwe wa Ujiji.

 

Meya huyo wa manispaa ya Kigoma Ujiji alisema kuwa binafsi aliamua kulivalia njuma vitendo vya ushoga na kuwafuata baadhi ya watu wanaotuhumiwa kwa vitendo hivyo lakini alishangazwa na majibu ya watu hao kumtaka asiwafuatilie  kwani miili wanayotumia kufanya hivyo ni ya kwao na wamepewa na Mungu


 Kwa upande wake Kiongozi wa Baraza kuu la Waislam mkoa Kigoma, Shekhe Harun Shaharawi alisema kuwa mmomonyoko wa maadili ya vitendo vya ushoga, ubakaji na ulawiti vimeufanya mji wa Ujiji ambao ulikuwa ukisifika kwa ustaarabu na maadili ya kiafrika kwa sasa umechafuka ikiwemo kufanyika kwa sherehe za Kitaifa za mashoga mambo ambayo yanaharibu maadili na mila za mji huo.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI