Baada ya kutoroka kwao Namibia (ikiitwa South West Africa) kwa njia za panya hadi Botswana, aliendelea na safari hadi Zambia. Akiwa Zambia aliona kuwa hana utulivu sawasawa. Aliendelea na safari tena mbele.
Solomon aliingia mjini Mbeya, Tanzania, mwaka 1974 akiwa hoi bin taabani. Alipokelewa na wenyeji wake waliotangulia, kamanda Peter Nanyemba na Thobias Hainyeko. The Hashim Mbita Project ya SADC inaeleza kwa kina uwepo watu kutoka Namibia, Zimbabwe, Msumbiji ndani ya Mkoa wa Mbeya.
Solomon alianza mafunzo ya kijeshi Mbeya lakini baadae alihamishiwa kambi ya Kongwa, Mkia wa Dodoma. Akiwa Dodoma alipata mafunzo hayo kwa undani zaidi chini ya askari wa JWTZ ili akirudi aungane na wenzake kuikomboa nchi yao iliyokuwa ikitawaliwa na Afrika Kusini.
Baada ya kumaliza kwa mafunzo ya kijeshi Dodoma, alipata nafasi ya kwenda Korea Kaskazini kuongeza mafunzo ya mwaka mmoja kuwa afisa wa jeshi. Alirudi Dodoma na kupanga mikakati ya kurudi Namibia na wengine waliokuwa kundi moja, huku wengine wakibaki Dodoma.
Baada ya uhuru wa taifa hilo [Namibia] Solomon aliteuliwa kuwa CDF wa pili wa Namibia baada ya kamanda Dimo Hamaambo ambaye naye alifunzwa kijeshi Tanzania. Sam Nujoma aliwaamini askari wa Tanzania kwa mafunzo waliyotoa kwa askari wake hao.
Agosti 11 mwaka 2025 Solomon Yesu Hawala alifariki dunia. Uwezo wake wa kazi ya jeshi ni alama ya wazi ya juhudi za jeshi la Tanzania.






0 Comments