Header Ads Widget

FDH YAPOKEA MSAADA WA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 20 WA VIFAA SAIDIZI KWA WATU WENYE ULEMAVU


 Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima App Dodoma

BENKI ya NMB imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watu wenye ulemavu mkoania hapa, ikiwamo mafuta maalum kwa ajili ya kujikinga na mionzi ya jua inayosababisha saratani ya ngozi kwa watu wenye ualibino.

Msaada huo umekabidhiwa kwa Taasisi inayojihusisha na masuala ya watu wenye ulemavu ya mkoani hapa ya Foundation For Disabilitie Hope (FDH).

Meneja wa NMB, Kanda ya kati Janeth Shangwe, akikabidhi msaada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa FDH, Maiko Salali alisema tukio hilo ni sehemu ya kutekeleza takwa na taasisi kuresha kwa jamii kile wanachokipata (CSR).

“Sisi kama NMB, kutoa msaada kwa jamii imekuwa ni jambo letu na tumekuwa tukithamini watu wa aina mbalimbali, tulipo pata maombi yenu kuwa mnahitaji vifaa kwa ajili ya kujingia na mionzi ya jua mara moja tuliona kuna umuhimu mkubwa kushirikiana na tutumie sehemu ya faida ambayo tunaipata kwa ajili ya kuleta msaada huu," Amesema.

Na kuongeza "Tunaamini kwa namna moja ama nyingine nyinyi kama Foundationa For Disabilities Hope hapa Dodoma mtaufikisha msaada huu kwa wengi ambao wanauhitaji na vitu hivi,”alisema.

Aidha, alisema MNB, wamekuwa karibu na jamii kwa kuweka namna sahihi ya kusaidia makundi mbalimbali katika jamii katika sekta ya elimu pamoja na afya.

Kadhalika, amesema vifaa walivyotoa ni pamoja na mafuta ya kujikinga na na mionzi ya jua 200, kofia za jua 200 pamoja na miwani ya jua 200 vyote vikiwa na thaani ya Sh. milioni 20.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa FDH, Maiko Salali, aliishkuru NMB kwa namna ambavyo imekuwa ikigusa makundi ya watu wenye ulemavu.

“Kupitia msaada huu mmerejesha matuamani kwa watu wenye ulemavu msaa huu kwetu sisi watu wenye ualibino mmetusaidia kuongeza kiwango cha kuishi sisi watu wenye ualibino tunakabiliwa na changamoto ya saratani  ya ngozi adui yetu namba moja ni jua,”alisisitiza Salali

Amesema, mionzi ya jua inapowapiga kwenye ngozi wanatokwa na vidonda ambavyo badae vinakwenda kusababisha saratani ya ngozi.

“Hivyo hivi vifaa vya kujikinga na mionzi ya jua vinakwenda kuimarisha maisha yetu na kuweza kushiriki katika kulijenga taifa letu,”amesema

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI