Header Ads Widget

DHORUBA YA MCHANGA IRAQ YAACHA WENGI NA MATATIZO YA KUPUMUA

 


Zaidi ya watu elfu moja wameachwa na matatizo ya kupumua baada ya dhoruba ya mchanga kukumba maeneo ya kati na kusini mwa Iraq, maafisa wa afya walisema.

Afisa mmoja katika jimbo la Muthanna aliripoti kwa shirika la habari la AFP takriban visa 700 vya kile walisema ni kukosa hewa.

Kanda zilizoshirikishwa mtandaoni zilionyesha maeneo yakiwa yamefunikwa na ukungu mnene wa rangi ya chungwa, huku vyombo vya habari nchini humo vikiripoti kukatika kwa umeme na kusimamishwa kwa safari za ndege katika baadhi ya maeneo.

Dhoruba za vumbi ni za kawaida nchini Iraq, lakini baadhi ya wataalam wanaamini kuwa zinaongezeka mara kwa mara kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Watembea kwa miguu na polisi walivaa barakoa kujikinga na vumbi na wahudumu wa afya walikuwa kwenye eneo la tukio kusaidia watu wenye shida ya kupumua, kulingana na AFP.

Hospitali katika jimbo la Muthanna kusini mwa Iraq zilipokea angalau "visa 700 za kukosa hewa", afisa wa afya wa eneo hilo alisema.

Zaidi ya watu 250 walipelekwa hospitalini katika jimbo la Najaf, na wagonjwa wasiopungua 322 wakiwemo watoto pia walipelekwa hospitali katika jimbo la Diwaniyah.

Watu wengine 530 waliripoti kuwa na matatizo ya kupumua katika majimbo ya Dhi Qar na Basra.

Mamlaka zililazimika kufunga viwanja vya ndege katika majimbo ya Najaf na Basra.

Iraq imeorodheshwa na Umoja wa Mataifa kama moja ya nchi tano zilizo hatarini zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa huku ikikumbana na dhoruba za mchanga, joto kali na uhaba wa maji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI