Utawala wa Trump umesema unazuia zaidi ya $2bn (£1.5bn) fedha za serikali kwa Chuo Kikuu cha Harvard, saa chache baada ya chuo hicho cha wasomi kukataa orodha ya matakwa kutoka Ikulu ya White House.
"Taarifa ya Harvard leo inaangazia kile ambacho kimejitokeza kuwa tatizo katika vyuo na vyuo vikuu vya kitaifa," Idara ya Elimu ilisema katika taarifa.
Ikulu ya White House ilituma orodha ya matakwa kwa Harvard wiki iliyopita ambayo ilisema ipo kwa ajili ya kupambana na chuki dhidi ya Wayahudi kwenye chuo kikuu. Ilijumuisha mabadiliko ya utawala wake, namna ya kuajiri na taratibu za usajili.
Harvard alikataa matakwa hayo siku ya Jumatatu na kusema Ikulu ya White House ilikuwa inajaribu "kudhibiti" jumuiya yake.
Ni chuo kikuu cha kwanza cha Marekani kukaidi shinikizo kutoka kwa utawala wa Trump kubadili sera zake. Mabadiliko makubwa yaliyotakiwa na Ikulu ya White House yangebadilisha shughuli zake na kutoa udhibiti mkubwa kwa serikali.
Rais Trump amevishutumu vyuo vikuu kwa kushindwa kuwalinda wanafunzi wa Kiyahudi wakati vyuo vikuu kote nchini vilipokumbwa na maandamano ya kupinga vita huko Gaza na uungaji mkono wa Marekani kwa Israeli mwaka jana.
0 Comments