Header Ads Widget

AKILI BANDIA "AI"KUTUMIKA KUBORESHA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

 

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima APP Dodoma 

WAZIRI wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi ,Vijana,Ajira na watu Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amesema Nafasi ya akili Mnemba na Teknolojia za kidigitali katika mapinduzi ya usalama na afya kazini kunalenga kuhamsisha na kuwakumbusha waajiri kuanza kujiandaa kutumia katika uzalishaji na utoaji huduma bora. 


Ameyasema hayo leo Aprili 23 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu siku ya kimataifa ya Usalama na Afya  Mahala pa kazi duniani huku akisisitiza kuwa matumizi ya akili Bandia (AI) na Teknologia ya kidigitali kazini ni eneo ambalo linabadilisha kwa kasi namna utendaji kazi unavyofanyika, kuwasilianana hata kulinda usalama kazini. 

"Teknolojia hii imeleta mabadiliko chanya mengi na baadhi ya mabadiliko hayo ni kama vile mshine na mifumo inayotumia akili mnemba kufanya kazi  haraka, kwa usahihi mkubwa na bila kuchoka" Amesema Ridhiwani


Na kuongeza "Roboti na mifumo ya kidigitali sasa kufanya kazi hatarishi ambazo zamani zilikuwa zikifanywa na binadamu hivyo kuwaepusha wafanyakazi na ajali, kusaidia kugundua hatari kama vile gesi hatari au moto mapema zaidi kuliko binadamu" Amesema


Aidha ameeleza faida za matumizi ya akili mnemba na kubainisha changamoto kadhaa zinazoweza kujitokeza wakati wa matumizi ya mashine zinazotumia akili mnemba. 


"Hivyo jamii itambue kwamba matumizi ya akili mnemba na teknolojia hayamaanishi kupotea kwa ajira zote bali yanaleta mabadiliko katika aina ya ajira" 


Hata hivyo amebainisha kwamba matumizi ya teknolojia hizo yanaleta ongezeko la mahitaji ya wataalam wa teknolojia, mafundi wa mitambo ya kisasa, na wasimamizi wa taarifa na mifumo ya akili mnemba. 


"Hii inahitaji mipango ya mafunzo na kujenga uwezo mpya kwa wafanyakazi wa sasa na wabaadae"


Akizungumzia kuhusiana na maadhimisho siku ya  usalama na afya mahala pa kazi inayotarajiwa kufanyika aprili 28 mkoani Singida amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wanaendesha kampeni maalum za uhamasishaji kupitia shughuli mbalimbali yakiwamo mafunzo ya usalama na afya miongoni mwa makundi mbalimbali yakiwemo wajasiliamali wadogo na watu wenye ulemavu. 


Pia amesema kutakuwa na maonyesho ya usalama na afya mahali pa kazi, bonanza la michezo, kuandaa tuzo ya kuyatambua maeneo ya kazi yanayotekeleza vyema sheria na 5 ya usalama na afya mahala pa kazi, na pia kliniki ya uchunguzi wa afya za wafanyakazi. 


"Hivyo nawahamasisha wafanyakazi kutoka maeneo mbalimbali siku ya kilele na wana singida kujumuika katika siku hiyo ili kutafakuri juu ya hali ya usalama na afya mahala pa kazi pamoja na kuwakumbuka wafanyakazi walioumia ama kupoteza maisha wakiwa wanatekeleza majukumu yao"


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI