Na, Titus Mwombeki- Habari na Matukio App Kagera.
Watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Kagera wameanza kupatiwa mafunzo maalum kuhusu utambuzi na utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa hemophilia.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na timu ya madaktari bingwa pamoja na wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, ikiongozwa na Dkt. Stella Rwezaula, Rais wa Chama cha Hemophilia Tanzania na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu kutoka Muhimbili.
Mafunzo haya yamewaleta pamoja wataalamu wa afya kutoka hospitali za wilaya zote za Kagera pamoja na baadhi ya vituo vya afya, lengo likiwa ni kuwawezesha kutambua wagonjwa wa hemophilia na kuwapatia matibabu stahiki.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Dkt. Stella Rwezaula alisema kuwa mpango huu ni sehemu ya jitihada za kuimarisha huduma za afya kwa wagonjwa wa hemophilia nchini, hasa wale walioko mikoani.
"Tunataka kuhakikisha wagonjwa w
a hemophilia wanapata huduma za matibabu kwa ukaribu zaidi.
Ndiyo maana tumeleta mafunzo haya ili wataalamu wa afya wa hapa Kagera wawe na ujuzi wa kutosha wa kuwahudumia wagonjwa,"
Aidha, Dkt. Rwezaula alitangaza kuwa kesho, Machi 20, 2025, kliniki maalum ya hemophilia itazinduliwa rasmi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa, Bukoba.
"Kliniki hii ni hatua kubwa kwa wagonjwa wa himofilia katika mkoa wa Kagera, kwani hapo awali walilazimika kusafiri hadi mwendo mrefu kwenda Hospitali ya Kanda Bugando na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Sasa huduma zitapatikana hapa hapa Bukoba," aliongeza.
Samabamba na hilo amerishukuru shirika la Nov Nordisk hemophilia foundation kwa msaada wao mkubwa wa kuendelea kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma hii.
0 Comments