Header Ads Widget

KATIKA KUADHIMISHA WIKI YA MAJI KAMPUNI YA TBL IMEJIPANGA KUJIDHATITI KATIKA UHIFADHI WA MAJI.

 

Na,Jusline Marco;Arusha

Kampuni ya Uzalishaji Bia Tanzania TBL leo imeungana na mataifa mbalimbali kuadhimisha siku ya maji Duniani kwa kuthibitisha dhamira yake ya kuhakikisha inasimamia matumizi endelevu ya maji ndani na nje ya shughuli zake za uzalishaji.


Mkurugenzi wa Masuala ya Kisheria na Mahusiano kutoka Kampuni ya TBL Bi.Neema Temba akizungumza na waandishi wa habari katika kuadhimisha wiki ya maji kuelekea siku ya Maji Duniani,amesema TBL inatambua umuhimu wa uhifadhi wa rasilimali za asili kama nguzo kuu ya maendeleo endelevu.


Amesema TBL kama sehemu ya juhudi zinazoendelea imeimarisha nafasi yake kama mtetezi wa matumizi bora na uhifadhi wa rasilimali za asili ikizingatia zaidi uendelevu wa maji ambapo imeendelea kusisitiza umuhimu wa maji katika shughuli za viwandani na ustawi wa jamii.


Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita TBL imepunguza matumizi ya maji katika shughuli zake za uzalishaji kwa takribani asilimia 30 kupitia uwekezaji katika teknolojia za urejeleaji wa maji na kupunguza upotevu ambapo mafanikio hayo yametokana na uwekezaji katika teknolojia za urejeshaji wa maji,uboreshaji wa mifumo ya uzalishaji na bidii kubwa ya wafanyakazi.


Akifungua hafla hiyo ya Wiki ya Maji Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Mkude ameipongeza kampuni hiyo kwa juhudi zake za kuhakikisha matumizi bora ya maji yanazingatiwa na uwekezaji wake katika suluhisho endelevu zinazonufaisha kiwanda na jamii inayoihudumia.

Ameongeza kuwa mahitaji ya maji kwa siku katika wilaya ya Arusha ni takribani ujazo wa qubick meter 18381 .12 ambapo kufikia mwaka 2017 kiwango cha usambazaji kilikuwa qubic meter 11580 kwa siku sawa na asilimia 64 .5 ambapo amesema  hali inayopelekea kuwa na wakazi asilimia 35.5 wasiokuwa na maji safi na salama.


Mkude ameeleza kuwa upungufu huo wa maji unaonyesha kuwepo kwa umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika usimamizi wa maji na miundombinu bora ambapo amesema ni muhimu kuwekeza katika teknolojia za kisasa za kuhifadhi maji ,kuboresha miundombinu na kuhakikisha tabia endelevu za utunzaji wa vyanzo vya maji unakuwepo.


Sambamba na hayo amesema katika kuadhimisha wiki ya maji ni vyema kuweka upya dhamira ya kusimamia maji kwa njia endelevu kwa kushirikiana na kutumia ubunifu kusudi kuweza kuhakikisha kila mkazi wa Arusha anapata maji safi na salama ili kujenga maisha bora yenye afya kwa wote.

Naye Injinia John Jonas Kasambili kutoka Shirika la kuhifadhi Mazingira Duniani WWF Tanzania ambaye ni msimamizi wa mradi wa Dar es salaam Water security unaofadhiliwa na kampuni ya AB Inbev amesema katika kuadhimisha wiki ya maji mradi huo umelenga kuboresha na kutunza rasilimali za maji ambapo ameyataka makampuni binafsi na jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa kuhakikisha wanashiriki katika kutunza rasilimali maji na kuwa endelevu.


Hafla hiyo ya Wiki ya Maji imeambatana na mijadala imahususi inayohusu nafasi ya ubunifu katika kuounguza matumizi yw maji katika shughuli za viwandani ikiwa ni dhamira ya TBL kupunguza athari za mazingira na kukuza matumizi bora ya rasilimali kwa muda mrefu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI