Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma
RAIS wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza ufadhili, ujenzi wa miundombinu ya kisasa na ushirikiano wa kimataifa uliowezesha mafanikio makubwa katika sekta ya Michezo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha na waandishi wa habari kueleza utekelezaji wa Baraza hilo kwa serikali ya awamu ya sita.
Amesema ukarabati mkubwa wa uwanja wa Benjamin Mkapa umegharimu shilingi Bilioni 31 za Kitanzania.
Amesema ujenzi wa uwanja mpya wa michezo Arusha ambao utagharimu shilingi Bilioni 338 hadi kukamilika kwake.
Amesema Ujenzi wa uwanja mpya wa michezo Dodoma unaotarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni utagharimu shilingi Bilioni 310.
Pia ameeleza kuna ujenzi wa viwanja vya mazoezi ikiwemo Gymkhana, Leaders Club,TIRDO, Law School na uwanja wa Farasi hadi kukamilika vitatumia shilingi Bilioni 21.
Aidha katika hatua nyingine Amesema Serikali imeondoa kodi ya nyasi bandia, hali iliyosaidia uwepo wa viwanja katika ngazi za Halmshauri na kusaidia vijana wengi kushiriki katika michezo
Amesema Tanzania imefanikiwa kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Michezo wenye jukumu la kuwezesha timu za Taifa, kutoa mafunzo kwa wataalamu wa michezo, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya michezo, kununua vifaa vya michezo na kuendeleza vipaji.
"Tumefanikiwa kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia kwa timu ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu na mpira wa miguu kwa wanawake chini ya miaka 17 nchini India mwaka 2022," Amesema Katibu Mtendaji huyo
Hata hivyo amesema Mchezo wa mpira wa miguu umepata mafanikio makubwa kutokana na hamasa ya goli la Mama ambayo imechochea klabu za Simba na Yanga, sambamba na timu za taifa kufanya vizuri.
Amesema katika upande wa mchezo wa gofu kwa wanawake mwaka 2022, timu ya Taifa ya wanawake ilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya All Afrika Challenge Trophy.
"Mchezo wa riadha umepeperusha vizuri bendera ya Tanzania kimataifa na kuipa Tanzania fursa ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya vijana ukanda wa Afrika Mashariki chini ya miaka 18 na 21 (EARR) ambapo Tanzania ilimaliza nafasi ya pili na tatu, " Amesema.
" Tunajivunia kwani Tanzania imekuwa ikifanya vizuri katika mchezo wa Kriketi mwaka 2024, imeweza kushinda mashindano ya ICC Mens T20 World Cup Sub Regional Africa Qualifier na kisha ikafanikiwa kushinda tena katika mashindano ya Mens ICC U 19 World Cup Qualifier Africa Division 2," Amesema Katibu Mtendaji huyo
Kwa upande wa michezo ya watu wenye ulemavu nayo imekuwa ikiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa na kufanya vizuri ikiwemo katika mchezo wa tenesi wa viti mwendo na mpira wa miguu.
0 Comments