Header Ads Widget

MASHIRIKA YASIYO KUWA YA KISERIKALI YATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA KANUNI TARATIBU NA SHERIA


Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kiseo Nzowa, azitaka taasisi na mashirika binafsi kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni, na taratibu zilizopo katika utekelezaji wa shughuli zao.


Amesema hayo wakati alipokuwa akifungua mkutano wa viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali uliofanyika mkoani Kilimanjaro.


Amesema kuwa ni muhimu kwa mashirika na taasisi binafsi kufuata miongozo ya kisheria ili kuepuka kuvunja sheria na kuleta changamoto kwa jamii na serikali. 

"

Ni muhimu kwa mashirika na taasisi binafsi kufuata miongozo ya kisheria ili kuepuka kuvunja sheria na kuleta changamoto kwa jamii na serikali."


Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini, Mwantumu Mahiza, ameyataka mashirika hayo (NGOs) kuhakikisha yanafanya kazi kwa mujibu wa malengo yao ya usajili na kuacha kuhamasisha ajenda zinazokiuka maadili ya Kitanzania.


Kila shirika lililosajiliwa lifanye kazi kwa mujibu wa lengo lake. Uzoefu umeonyesha kuwa baadhi ya mashirika yamesajiliwa kwa shughuli fulani, lakini utekelezaji wake unaenda kinyume na maadili yetu kwa kuingiza ajenda zisizo sahihi," amesema Mahiza.


Washiriki walioshiriki katika mkutano huo wameiomba serikali kutoa ushirikiano pale wanapohitaji .


"Tunaomba serikali kutoa ushirikiano zaidi pale tunapohitaji ili kuhakikisha miradi yetu inafanikiwa na kuwa na manufaa kwa jamii."


Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali 467 kwa mkoa wa Kilimanjaro na kati ya hayo mashirika yaliyosajiliwa ni 177 .




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI