Header Ads Widget

RC ANDENGENYE AONYA WAFANYABIASHARA KIGOMA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amekemea wafanyabiashara wa mkoa huo wanaoingiza bidhaa nchini bila kufuata taratibu wa kulipa ushuru (Magendo) wamekuwa wakiikosesha serikali mapato na hivyo kutoa onyo kwamba adhabu kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.


Andengenye alisema hayo katika hafla ya utoaji tuzo kwa wafanyabiashara wa mkoa Kigoma iliyoandaliwa na Mamlaka ya mapato kutambua mchango mkubwa wa wafanyabiashara hao katika kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati hivyo kuifanya mamlaka hiyo kufikia lengo la ukusanyai.

Pamoja na kutoa onyo hilo  Mkuu wa wilaya Kigoma,Dk.Rashid Chuachua ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma alisema kuwa anaipongeza TRA kwa kazi kubwa ya kukusanya kodi na kufikia malengo ya ukusanyaji yaliyowekwa jambo ambalo linaifanya serikali kuweka mazingira wezeshi ya kuifanya mamlaka hiyo kutimiza malengo yake kwa ufanisi.


Chuachua alisema kuwa ukwepaji kodi sambamba na wafanyabiashara wasiotumia mashine za kielektroniki kumesababisha serikali kupoteza mapato hivyo amepota onyo kwa wafanyabiashara wanaofanya hivyo kuacha mara moja huku akiipongeza TRA kuongeza ukusanyaji mapato ambako kumeifanya serikali kutekeleza miradi mikubwa Kwenda kwa wananchi.

Akizungumza katika hafla hiyo Naibu Kamishna wa forodha na ushuru wa bidhaa TRA Makao Makuu, Julieth Nyomolelo amesema kuwa uingizaji wa bidhaa nchini bila kulipiwa kodi kwa njia ya magendo  imekuwa changamoto kubwa ambayo inavuruga malengo ya mamlaka hiyo katika kufikia lengo la ukusanyaji mapato nchini.

Naibu Kamishna wa forodha na ushuru wa bidhaa alisema kuwa ulipaji kodi kwa hiari kwa kufuata taratibu za kisheria kulingana na biashara iliyofanyika inatija kubwa katika kuongeza makusanyo ya mamlaka hiyo sambamba na kufikia au kuvuka lengo lililoweka hivyo ametoa wito kwa watu wote kufuata taratibu na kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati.


Akizungumzia utoaji huo wa tuzo alisema kuwa unalenga kuwatambua na kuwatia moyo wafanyabiashara wanaolipa kodi kwa hiari na kwa wakati kwani wamesaidia kuondoa usumbufu wa mamlaka hiyo kutumia muda mwingi, rasilima na nguvu nyingi kuwafuata walipa kodi ili kutimiza wajibu wao huo wa kisheria.


Awali Meneja wa TRA mkoa Kigoma,Beatus Mchota alisema kuwa Pamoja na changamoto ya uingizaji bidhaa kwa njia ya magendo kuvuruga malengo yao pia wafanyabiashara wasiotumia mashine za kielektorniki wameongeza changamoto kubwa katika suala la ukadiriaji na ulipaji kodi kwa hiari kwani sehemu kubwa ya mauzo yao yanakuwa hayaingii kwenye hesabu za biashara waliyofanya.

Meneja huyo wa TRA mkoa Kigoma alisema kuwa Pamoja na changamoto mbalimbali zinazojitokeza lakini mamlaka hiyo mkoani Kigoma imepata mafanikio katika ukusanyaji ambapo kwa kipindi hicho imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 15.4 kati ya lengo la kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 15.9 na kwamba elimu na mikutano wanayofanya imesaidia wafanyabiashara kufuata taratibu na kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati.


Mmoja wa wafanyabiashara waliopewa tuzo kwenye hafla hiyo, Kilahumba Kivumo alisema kuwa mabadiliko ya utendaji ya maafisa wa TRA ambayo yametokana na vikao vya mara kwa mara wanavyofanya imekuwa chachu kwa wafanyabishara kulipa kodi kwa hiari na kuwaita maafisa hao kuwapa ushauri badala ya kuwakimbia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI