Header Ads Widget

KWA KAZI HIZI, KWELI SAMIA MITANO TENA – ISRAEL SALUFU, KADA WA CCM

 


Na Matukio Daima Media 

WAKATI tayari Chama Cha mapinduzi (CCM)kikiwa kimepitisha azmio la mgombea wake wa nafasi ya Urais mwaka huu kuwa ni Dkt Samia Suluhu Hassan makundi yanayobariki uamuzi huo yazidi kuongezeka na kuunga mkono kwa asilimia 100.

Ifahamike kuwa  Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa za maendeleo ambazo zinadhihirisha uwezo wake wa uongozi.


 Leo Katika kipindi Cha Tanzania ya Leo kinachorushwa na Matukio Daima Tv Israel Salufu, kada wa CCM kutoka kijiji Cha Ilula wilaya ya Kilolo mkoani Iringa anasema utendaji wa Rais Samia unatoa sababu ya msingi kwa Watanzania kumpa tena kipindi kingine cha miaka mitano ili aendelee na juhudi zake za kujenga taifa.

Kuwa katika sekta ya miundombinu, serikali yake imefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa kama barabara za kisasa, madaraja, na reli ya kisasa ya SGR, ambayo inaboresha usafiri wa abiria na mizigo. Hii inasaidia kuchochea uchumi wa nchi kwa kurahisisha biashara na uwekezaji.

Salufu alisema ujenzi wa viwanja vya ndege katika mikoa mbalimbali ukiwemo Uwanja wa Ndege Iringa unazidi kuboresha sekta ya usafiri wa anga.

Hata hivyo alisema katika sekta ya elimu, Rais Samia amehakikisha watoto wa Kitanzania wanapata elimu bora kwa kuongeza bajeti ya elimu, kujenga madarasa, kuajiri walimu wapya, na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa wingi zaidi.


" Hili limeongeza fursa za vijana kupata maarifa yatakayowasaidia kujenga taifa lenye nguvu"

Salufu alisema Sekta ya afya nayo imepiga hatua kubwa chini ya uongozi wake.

 Hospitali kama Ile  ya Kilolo  na vituo vya afya vimejengwa katika maeneo mengi nchini, na huduma za matibabu zimeimarishwa kwa kuongeza dawa, vifaa tiba, na kuajiri wahudumu wa afya. 

Pia, serikali yake imeendelea kuboresha bima ya afya kwa wote ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata matibabu bila kikwazo cha gharama.

Katika sekta ya kilimo Salufu alisema Rais Samia amewekeza kwa wakulima kwa kuwapatia pembejeo kwa wakati, kuboresha masoko ya mazao, na kuhimiza kilimo cha kisasa kupitia teknolojia za umwagiliaji.

Kuwa  inasaidia kuongeza uzalishaji wa chakula na kukuza uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla.

Aidha alisema Rais Samia amejitahidi kukuza nafasi za ajira kwa vijana kwa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.


" Serikali yake imeweka mkazo katika sekta ya viwanda ili kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na kuzalisha bidhaa zinazouzwa ndani na nje ya nchi mikopo kwa wajasiriamali na wanawake imeimarishwa ili kuhakikisha makundi yote yanapata fursa za kiuchumi"


Israel Salufu (kulia) akiwa nchini China 

Katika diplomasia, Tanzania chini ya Rais Samia imeimarisha uhusiano wa kimataifa kwa kuvutia wawekezaji wa kigeni, kushiriki mikutano mikubwa ya kimataifa, na kuimarisha mahusiano na mataifa mbalimbali kwa manufaa ya Watanzania.



Salufu ambae amesomea Maendeleo ya Kimataifa na mahusiano ya Kimataifa (PhD in international Development and Cooperation ya University of international business and Economic -Beijing china   alisema kutokana na mafanikio haya, Watanzania wengi wanaamini kuwa Rais Samia anastahili kupewa kipindi kingine cha miaka mitano ili aendelee kuleta maendeleo. 

 Salufu aliwataka   wanachama wa CCM kuelewesha wasioelewa kazi hizo na kuziunga mkono   juhudi za serikali chini ya Rais Dkt Samia kwa maendeleo ya nchi kuwa ndio maana kwa kazi hizi, kweli Samia Mitano Tena!

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI