Header Ads Widget

“VALENTINE WEEKEND GATEAWAY NA TANAPA” NDANI YA HIFADHI YA TAIFA KISIWA CHA SAANANE

Maandalizi ya hafla ya kilele cha Kampeni ya Valentine Weekend Gateway na TANAPA yakamilika ndani Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane, huku watalii wakimiminika kushiriki tukio hilo linalotarajiwa kufanyika jioni ya Februari 15, 2025. 

Wageni 45 kutoka Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama, ambao ni watumishi wa Umma, wametembelea Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane na kushiriki kampeni kwa kutembelea Hifadhi na kujionea vivutio vya utalii kama wanyama aina ya Simba, Tausi, Swala, kenge pamoja na madhari nzuri ya miamba iliyopo ndani ya Hifadhi.

Wakati huo huo, maandalizi ya hafla ya jioni yanaendelea kwa hatua za mwisho, ambapo kambi ya kulala watalii imepambwa kwa mandhari ya kuvutia, vyombo vya usafiri wa maji vimeandaliwa kwa ajili ya safari za boti, na eneo la burudani limewekwa tayari kwa ajili ya sherehe ya wapendanao itakazojumuisha muziki, chakula cha jioni, na tafrija maalumu chini ya anga la kuvutia la Kisiwa cha Saanane.

Kaa tayari kufuatilia kupitia Mitandao yetu ya Kijamii @tanzaniaparks @tanapaupdates (Instagram) @TANAPA MEDIA (Youtube) na Chaneli ya WhatsApp. 










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI