Header Ads Widget

MVUA YALETA MADHARA MAKUBWA WINOME KILOLO



Na Matukio Daima media,Kilolo

Mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali imeharibu mashamba zaidi ya ekari 50 ya wakulima na kuezua nyumba 3  za watu katika kijiji cha Winome wilaya ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa.

Akizungumza na MATUKIO DAIMA MEDIA Mwenyekiti wa kijiji cha Winome Bw. Obby Madafu alisema kuwa mvua hiyo ilinuesha Jana February 9, 2025 kuanzia majira ya saa 8:00 alasiri hadi sasa 10:30 jioni.

Bw. Madafu alisema kuwa pamoja na MADHARA hayo yaliyojitokeza, hakuna vifo vya watu na wanyama vilivyotokea katika tukio hilo.

Alisema kuwa katika kijiji cha Winome mvua hiyo ya upepo mkali iliambatana na mawe ambapo imedondosha mti mkubwa ambao ilikuwa ni Nembo ya kijiji cha Winome kwa muda mrefu.

Bw. Madafu alisema kuwa katika tukio hilo watu walipata taharuki kubwa kutokana na hali ya upepo mkali ambao hujawahi kutokea.

Aliwataja watu ambao nyumba zao zimedondoka kuwa ni Adelisi Kadinde, Jacob Lusinde na Budwana Kiyeyeu kuwa nyumba zao zimedondoka kabisa ambapo nyumba nyingine 20 zimeezuliwa nusu yake.

Mwenyekiti wa kijiji cha Winome ameiomba Serikali ya wilaya na mkoa kutoa misaada ya haraka katika janga hilo lililowakuwa wananchi wa kijiji cha Winome ili kuwasaidia makazi katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na MATUKIO DAIMA, baadhi ya wananchi wakazi wa Winome walisema kuwa mvua iliyonyesha Jana ilikuwa ya kutosha sana kiasi kwamba kulikuwa na taharuki kubwa sana kwa wananchi.

"Hali ya upepo na mvua kubwa ya mawe iliyonyesha ilileta taharuki kubwa sana kwa wananchi wakazi wa Winome, tukio la kuondoka nyumba, kuharibu mashamba na kuondoka kwa mti mkubwa ambao ni Nembo ya kijiji umeishi zaidi ya Miaka 100 tumeshangaa sana kuondoka ", alisema Bw. Stanislaus Kadinde.

Wananchi hao wameiomba Serikali kuwasaidia wahanga wa nyumba zilizodondoka kwa kuwapa misaada ya kujenga, kuezeka na kuwapa misaada ya chakula ili waweze kujikimu katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI