Muhadhiri Tuladega Tweve
NA.ZUHURA ZUKHERI
Ikiwa imezoeleka maadhimisho ya wiki ya Sheria kufanyika kila mwaka nchini Tanzania kwa Kila Kanda ya Kimahakama .
Mahakama kuu kanda ya Bukoba imeadhimisha kipekee kwa kutambua mchango wa vyombo vya habari kwa kuwapa vyeti maalumu vya pongezi hakika wamefanya jambo la kipekee sana.
Lakini pia ni jambo la fahari sana kwa Wana Iringa na watanzania wote wadau wa Matukio Daima media kushuhudia chombo cha habari cha Matukio daima kupokea cheti kinachoonesha kuwa mahakama kanda ya Bukoba chini ya Mhe. Immaculata Kajetan Banzi, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi katika Siku ya Sheria kwa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba.
Tuladega Tweve Muhadhiri msaidizi chuo kikuu kishiriki - Marian na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Kiswahili language Initiatives for Women Foundation (Kilaiwo Foundation)anasema Matukio Daima media tuzo hiyo ni Haki yake kwani ni Chombo kinachofanya vizuri sana .
"Imefurahishwa sana na matukio Daima Media kurusha matukio ya wiki nzima mubashara"
Kuwa kitendo cha kupokea tuzo hiyo ni heshima waandishi wa Chombo hiki chini ya mkurugenzi wake Francis Godwin na timu Nzima kwani jitihada kubwa Chombo hiki kimekuwa kinafanya ndani ya Iringa ambako ni chimbuko ,mikoa ya nyanda za juu kusini pia nchini Nzima kwa kuripoti mara kwa mara matukio ya mubashara.
"Hakika wana Iringa tumefurahishwa sana na hilo na pia hata Kanda zingine zaweza kujfunza kutoka kanda ya bukoba nazo zikawe na utaratibu huo wa pongezi kwa vyombo vya habari katika matukio mengine yatakayofuata maana jambo hilo linatengeneza daraja linalounganisha muhimili wa mahakama na jamii kupitia vyombo vya habari mbalimbali hususani Matukio Daima Media "
Pamoja na pongezi hizi toka kwa Muhadhiri msaidizi chuo kikuu kishiriki - Marian Tuladega Tweve pia wadau mbali mbali ndani ya mkoa wa Iringa wamepongeza heshima hii ya Matukio Daima media.
Kupitia kundi maarufu la mkoa wa Iringa linaloundwa na Wanakundi 1024 wakiwemo watu wa kada mbali mbali wameeleza kufurafishwa na heshima hiyo ambayo Chombo hiki kimepata.
mkurugenzi wa Matukio Daima media Francis Godwin amepongeza wote kwa pongezi zao pia ameupongeza uongozi wa Mahakama kuu Kanda ya Bukoba chini ya Jaji mfawidhi Immaculate Kajetan Banzi ,Said Mkasiwa, Naibu Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba na wafanyakazi wote wa Mahakama hiyo.
Alisema kuwa Matukio Daima Media Ina waandishi mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na kuwa wajibu Wao kuendelea kuhabarisha umma kwenye Matukio yote huku akiomba wadau kuendelea kutumia Matukio Daima media kutangaza shughuli zao.
Hata hivyo alisema anawapongeza waandishi wa Matukio Daima media mkoa wa Kagera wakiongozwa na Shamsa Mussa kwa kuwakilisha vema mkoa wa Kagera na kupelekea Chombo kupata heshima hiyo.
Aliwataka hata hivyo alisema Matukio Daima media ni mdau mkubwa wa gazeti la Raia Mzalendo linalotoka Kila Siku kwani wanafanya kazi kwa mashirikiano Makubwa hivyo wadau kutumia vizuri vyombo hivi kutangaza Matukio yao kwa kupiga simu 0754026299 namba ya Matukio Daima media.
0 Comments