Na Matukio Daima media
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema kuwa hafahamu kama majeshi yake yako Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mashariki mwa DRC ni eneo ambalo mapambano kati ya vikosi vya Jeshi la DRC (FARDC) na waasi wa Kundi la M23 yameshika kasi huku waasi hao wakidai kuushikilia Mji wa Goma nchini humo.
Mapigano kati ya pande hizo yanatajwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 700 huku zaidi ya 2,300 wakijeruhiwa
Katika mahojiano na CNN, Jumatatu Januari 3,2025, Kagame alipoulizwa iwapo kuna vikosi vyovyote vya Rwanda nchini DRC amejibu:
"Sifahamu," amesema Kagame, pamoja na kuwa yeye (Kagame) ni Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Rwanda
"Kuna vitu vingi ambavyo sivifahamu. Ila ukiniuliza kama kuna tatizo nchini Congo ambalo Rwanda inahusishwa na Rwanda itafanya kila iwezalo kujilinda nitakujibu asilimia 100," amesema.
0 Comments