Header Ads Widget

WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI TANAPA WAKAGUA MIRADI HIFADHI YA SAANANE


Na. TANAPA, SAANANE

Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) walitembelea Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane, Februari 03, 2025 kwa ajili ya ukaguzi wa miradi mbalimbali, kupata taarifa ya afya za wanyama, maendeleo ya Hifadhi na utendaji kazi.

Baada ya kupokea taarifa fupi ya Hifadhi hiyo wamepongeza utendaji kazi wa Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane hususani juhudi zinazofanywa katika kuongeza idadi ya watalii wa ndani, bodi hiyo ya wadhamini imeutaka uongozi wa hifadhi kuongeza jitihada kwenye kuongeza vivutio na kutangaza Hifadhi ili idadi ya watalii iongezeke zaidi.

Sambamba na kutembelea miradi ya Maendeleo pia, walipata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii, Mahema kwa ajili ya malazi ya watalii pamoja na Ikolojia ya hifadhi ikiwemo malisho ya wanyamapori. ‎







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI