Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Njombe imefanikiwa kumfikisha Mahakamani Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Lupembe Bi.Mary Ng'umbi na Kuhukumiwa Kifungo cha Mwaka mmoja Jela baada ya kupatikana na hatia ya Kushawishi na kupokea Rushwa kwa mzazi ili mtoto asiende Shule
Taarifa ya hukumu hiyo Imetolewa na Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Njombe Noel Mseo wakati akitoa taarifa ya Utendaji kazi wa Taasisi hiyo katika Kipindi cha Mwezi Oktoba hadi Disemba ambapo amesema Mtendaji Huyo alikutwa na Hatia kwa Makosa Mawili ya Kushawishi na Kupokea Rushwa ya Shilingi 100000 kati ya 250000 aliyoomba Kwa Bwana Zabron Kisakali ili kumsaidia kukwepa adhabu ya kosa la kutompeleka mtoto wake shule.
Kutokana na Hali Hiyo Kaimu Kamanda wa Takukuru ana toa wito kwa wazazi wenye tabia za kukatisha ndoto za watoto wao kwa kutowapeleka shule huku akitoa onyo kwa Maofisa wa Serikali wanaoshiriki vitendo hivyo.
Wananchi mkoani Njombe akiwemo Mohamed Milanzi,Angel Kivale na Tony Lyaruu wameonesha kukerwa na kitendo hicho huku wakiwataka viongozi wa aina hiyo wafutwe kazi mara moja.
Januaria 13, mwaka huu shule zote za msingi na sekondari zilifunguliwa huku serikali ikisisitiza wanafunzi wote kuripoti shle lakini baadhi yao mpaka sasa wanadaiwa kutoripoti kwa sababu mbalimbali ikiwemo wazazi kukosa michango na baadhi ya wazazi kuwazuia.
0 Comments