Header Ads Widget

WANAFUNZI WATOA NENO KWA RAIS SAMIA UJENZI SHULE MPYA YA SEKONDARI


 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mkabuye iliyopo wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wametoa shukrani zao kwa Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia ujenzi wa shule ya sekondari katika kata hiyo  hali iliyosababisha kuondokana na adha mbalimbali ikiwemo adha kubwa ya kutembea umbali mrefu Kwenda shule na kurudi.

Wanafunzi hao wametoa kauli hiyo kwa Rais Samia kwa timu ya waandishi wa Habari waliotembelea shule hiyo ambapo wamesema kuwa baada ya kuhamishwa kutoka shule ya awali ya Itaba Sekondari na kuanza masomo kwenye shule hiyo ya Mkabuye mwaka 2023 wanaamini serikali inawajali wananchi wake bila kubagua.

John Aborgast mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo ya Sekondari Mkabuye akizungumza shuleni hapo alisema kuwa wakati wanasoma shule ya sekondari Itaba adha ilikuwa kubwa sana maana walilazimika kuamka mapema asubuhi ili kutembea umbali wa Zaidi ya kilometa sita kufika shule hivyo hata usomaji wao ulikuwa na changamoto kubwa.






Naye Mwanafunzi Zelekia Herman ambaye alihamia shule hapo mwezi Mei mwaka 2023 wakiwa wanafunzi wa mwanzo kujiunga na shule hiyo ya Mkabuye alisema kuwa kwao imekuwa ukombozi mkubwa kwani adha ya kutembelea umbali mrefu na changamoto nyingine hasa kwao wasichana zimepungua.                      

Akizungumzia ujenzi wa shule hiyo Makamu Mkuu wa shule hiyo ya Sekondari ya Mkabuye, Mwl.Damiano Fubusa alisema kuwa serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 603 ambazo zimewezesha kujengwa kwa madarasa 13, jengo la utawala, maabara za sayansi, jengo la Maktaba na jengo la TEHAMA lenye vifaa vyote  ambapo alisema kuwa ujenzi huo umesaidia  kupunguza umbali, msongamano na changamoto za baadhi ya wanafunzi kupanga nyumba ili kupata wasaa mzuri wa kupata masomo jambo ambalo kwa sasa halipo tena.

Aidha kufuatia ujenzi wa shule hiyo Kaimu Afisa elimu Sekondari wa Halmashauri ya wilaya Kibondo, Respiuce Nkwaitabo alisema kuwa shule hiyo imejengwa kupitia mradi  wa kuimarisha elimu ya  Sekondari (SEQUIP) na kuifanya Halmashauri hiyo kuwa na shule 24 za sekondari na kwamba  ujenzi wa shule hiyo  imeongeza chachu ya wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kutokana na kuwepo kwa maabara za sayansi, Computer lakini pia imesaidia kuondoa utoro ambapo kwa sasa mahudhurio ya wanafunzi ni makubwa.

Mwisho.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI