DODOMA.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Saidi Jafo (Mb.) kwa mujibu wa Sheria Na. 23 ya 1980 Sura ya kwanza (1) (c) ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO), ameteua Wajumbe (5) wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa kwa Umma iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Viwanda na Biashara, Bi. Suzan Mshakangoto, 3 Februari 2025, amebainisha kuwa Uteuzi huo umeanza 29 Januari, 2025.
Wajumbe hao ni pamoja na:
i) Prof. Ismail Juma Ismail, Profesa Mshiriki kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma,
ii) Dkt. Abdallah Mrindoko Ally, Mhadhiri, kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania.
iii) Bi.Zaytun Kikula Mkurugenzi wa Utafiti, Miungano ya Kampuni na Uraghibishi kutoka Tume ya Ushindani.
Wengine ni,
iv) Bw. Erick Kitali Mkurugenzi wa TEHAMA, TAMISEMI; na
v) Bi. Ingrid M. Sanda kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.






0 Comments