Na Matukio Daima media
Mashindano ya Vunjabei Cup 2025 yameanza kwa kishindo, yakishirikisha jumla ya timu 120 kutoka maeneo mbalimbali.
Mashindano haya tayari katika hatua ya awali ya mtoano, timu 50 zimefanikiwa kufuzu na kuingia katika hatua inayofuata ya mashindano.
Ifuatayo ni orodha ya timu hizo pamoja na maeneo wanakotoka
- WASA FC (WASA)
- RENJAZI FC (LYAMGUNGWE)
- MAGULILWA FC (MAGULILWA)
- MGERA FC (MGERA)
- MIGOLI FC (MIGOLI)
- IZAZI KIDS FC (IZAZI)
- MBUGANI FC (MBUGANI)
- KISING'A FC (KISING'A)
- FEMA SPORTS (MAUNINGA)
- MKIMBIZI FC (MKIMBIZI)
- SUPER EAGLE FC (MLANDEGE)
- LUHOTA MIXTURE (LUHOTA)
- MGAMA FC (MGAMA)
- ILOLO UNITED (ILOLO MPYA)
- KIMANDE STARS (ITUNUNDU)
- WAKILI FC (MSHINDO)
- PENTAGON FC (MAKORONGONI)
- MORNING FIGHTER FC (ILALA)
- KITWIRU FC (KITWIRU)
- ST. DOMINIC SAVIO (NDULI)
- FRELIMO FC (KWAKILOSA)
- LUZERN FC (IGUMBILO)
- KALENGA FC (KALENGA)
- TANANGOZI FC (MSEKE)
- KIKONGOMA FC (ULANDA)
- SCOUT FC (MIVINJENI)
- IFUNDA COMBINE (IFUNDA)
- MAGUNGA FC (MABOGA)
- NZIHI FC (NZIHI)
- READ LEAF (LUMULI)
- SPANA FC (RUAHA)
- KIHESA FC (KIHESA)
- DREAM BOY (MTWIVILA)
- KIHANGA FC (KIHANGA)
- VIWENGI FC (KILOLO)
- FOX FC (KILOLO)
- TANESCO (MIYOMBONI)
- MAGIC SITE (MKWAWA)
- SADAN FC (MASAKA)
- SUMA JKT (GANGILONGA)
- ISAKALILO FC (ISAKALILO)
Kwa mujibu wa Katibu wa Chama cha Soka Manispaa ya Iringa, Yahaya Mpelembwa, mashindano haya yamekuwa na ushindani mkubwa, ambapo michezo ya awali ilichezwa kwa mtindo wa mtoano ili kupata timu hizo 50 bora ambazo sasa zitacheza kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Vunjabei, Fadhil Ngajilo, alieleza kuwa mashindano haya yameboreshwa kwa kiwango kikubwa, ambapo zawadi ya mshindi wa kwanza imeongezwa kutoka ng'ombe mmoja hadi shilingi milioni 10.
Pia, zawadi kwa mshindi wa pili na wa tatu zimeongezwa hadi shilingi milioni tatu na milioni mbili mtawalia.
Zawadi nyingine ni pamoja na shilingi laki tano kwa kikundi bora cha ushangiliaji, na tuzo kwa mwandishi bora, mchezaji bora, mfungaji bora, na kipa bora wa mashindano.
Mashindano ya Vunjabei Cup 2025 yamekuwa na msisimko mkubwa, yakileta pamoja timu kutoka maeneo mbalimbali na kuonyesha vipaji vya soka vilivyopo nchini.
Timu zilizofuzu zinaendelea na maandalizi kwa ajili ya hatua zinazofuata, huku mashabiki wakitarajia mechi za kusisimua na ushindani mkali.
TAZAMA TAARIFA YA HABARI KUHUSU VUNJABEI CUP BOFYA LINK HII
0 Comments