Header Ads Widget

MRADI WA UCHIMBAJI VISIMA VYA UMWAGILIAJI WATUA LINDI NA MTWARA MKANDARASI AKABIDHIWA SITE

 



Na Hadija Omary 


Lindi.....ZAIDI ya shilingi milioni 400 zinatarajiwa kutumika Katika Mradi wa uchimbaji wa Haidrolojia na uchimbaji wa visima 9 vya umwagiliaji Katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.


Akizungumza Katika makabidhiano ya Eneo na mkandarasi anaetekeleza Mradi huo JANIX CONSTRUCTION CO.LTD Leo February 6 huko  Katika kijiji cha Nkowe halmashauri ya Ruangwa  Mhandisi wa umwagiliaji Mkoa wa Lindi  Shamili karama amesema  Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa kwa miezi 6 kuanzia 21, 02,2025 na kukamilika august 20 2025.


"Mradi huu ni Utekelezaji wa Irani ya chama cha mapinduzi CCM ambapo Serikali ya awamu ya sita kupitia wizara ya kilimo iliagiza tume ya Taifa ya umwagiliaji kuchimba visima vya umwagiliaji na uwekaji wa  miundombinu ya umwagiliaji kwa umeme jua Kwa halmashauri sawa na visima 10 kwa kila halmashauri " alieleza Mhandisi Karama.


Amesema  kwa awamu hiyo ya Kwanza Katika Utekelezaji wa Mradi huo Mkoa wa Mtwara utahusisha visima 5 huku Mkoa wa Lindi ukipata visima 4 Katika vijiji vya Nkowe halmashauri ya Ruangwa, Kilangala A Manispaa ya Lindi,  Kilimahewa Mtama pamoja na Hangamwana Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.





Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma amemtaka Mkandarasi anaetekeleza Mradi huo wa uchimbaji wa visima vya umwagiliaji Mkoani humo kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kwa wakati uliopangwa na kwa viwango na ubora kwa mujibu wa mkataba.


" Tunafahamu huu Mradi ni Utekelezaji wa Irani ya chama cha mapinduzi CCM na Katika hili nisiwe muongo mwaka huu chama tuna jambo letu sasa kucheleweshwa kukamilika huu Mradi Kwa muda uliopangwa ni sawa na kukipigisha shoti chama cha mapinduzi na Mimi sitakubali" alisema Ngoma.

Kwa upande wake Jackson Mpole mkurugenzi wa kampuni JANIX CONSTRUCTION CO.LTD anaetekeleza Mradi huo amesema wamejipanga vyema kuhakikisha Mradi huo unakamilika kwa wakati na matumaini Yao ni kwamba kukamilisha kabla ya muda uliopangwa.


Baahi ya wanufaika wa Mradi huo wamesema Kukamilika kwa Mradi huo kutaongeza tija Katika kilimo chao kwani muda wa kulima utaongezeka kuliko Awali na hatimae kipato kitaongezeka 

" Kwa sasa Katika upatikanaji wa maji hakuna changamoto kubwa isipokuwa kipindi cha kiangazi tunapata shida katika upatikanaji wa maji ya kumwagilia bustani zetu hivyo kupitia Mradi huu ni wazi kwamba tutakuwa tumenufaika"  alisema Hawa Hassan Mmoja wa wanufaika

Mwishoo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI