Header Ads Widget

TUKIO LA UHAMAJI WA NYUMBU KWENDA KENYA, WATALII WAFURIKA HIFADHI YA SERENGETI


 


NA MWANDISHI WETU, SERENGETI

NI mafuriko ya watalii. Hivi ndivyo unavyoweza kusema ukifika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti husuan eneo la Seronera.  Hoteli zote zimejaa wageni. Magari ya kubeba watalii hazina idadi.


Ni mwendo wa ndege kutua na kuondoka, zikishusha na kupakia abiria wengi wakiwa ni raia wa kigeni wanaoingia na kutoka kwenye hifadhi ya Serengeti ambayo ni maarufu duniani kwakuwa na wanyama watano wakubwa.


Kaimu Mkuu wa hifadhi hiyo, Alex Choya alisema hayo Juni 20 mwaka huu 2025, ambapo alisema huu ni msimu mkubwa wa watalii (high sisson) kutoka kila pembe ya dunia kuja Tanzania hususani Serengeti kushuhudia tendo la maajabu ya wanyama nyumbu kuhama kutoka Serengeti kwenda Masai Mara nchini Kenya.


Choya alisema wanyama hao ambao huanza kujikusanya kwa makundi kutembea kuelekea Masai Mara huanza Katikati ya mwezi Juni hadi Julai kila mwaka ni mojawapo ya maajabu ya dunia yanayoipa upekee hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuchangia watalii wengi kuja Tanzania kushuhudia tukio hilo lisilokuwa la kawaida.


“Umaarufu mkubwa wa Hifadhi ya Serengeti ni uwepo wa wanyamapori wanaohama kutoka sehemu moja kwenda eneo lingine kama ilivyo kwa binadamu.


“Inakadiriwa nyumbu milioni 1.5 pamoja na wanyama wengine huama kwa ajili ya kwenda kutafuta chakula, maji na mazingira ya kuzaliana ambayo inajulikana zaidi kama ‘great migration’.”aisema Choya.


Mbali na hilo, Choya ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Utali wa hifadhi hiyo, alisema filamu iliyoandaliwa na Rais Samia Suluhu Hassan maarufu Royal Tour imekuwa kichocheo kikubwa cha kuongezeka kwa utalii katika hifadhi zote zinazosimamiwa na Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA).


Alisema tangu kuchezwa kwa filamu hiyo iliyolenga kuhamasisha utalii nchini, imekuwa kivutio na ksababisha ‘mafuriko’ ya watalii wanaojitokeza kutembelea hifadhi hiyo na kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo Serengeti.


Mhifadhi huyo alisema tangu kuzinduliwa kwa filamu hiyo Mei 7, 2022 Visiwani Zanzibar na baadaye nchini Marekani, hifadhi hiyo imeweza kutembelewa na watalii 1,334,054 na kati yao, 976,094 ni raia wa kigeni na 357,960 ni wale wa ndani.



Mbali na watalii wa nje, Kaimu huyo alisema kumekuwapo na mwitikio mkubwa wa viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kutembelea hifadhi hiyo, na katika siku za karibuni maaskofu, wachungaji na mashekhe na dini za asili wamekuwa wakitembelea hifadhi hiyo kwa lengo la kupumzika na kutafakari mambo mbalimbali ya Imani.


“ Kutembelea hifadhi kama hii yenye vivutio na maajabu mbalimbali ni tiba kubwa kwete afya ya akili, hivy kwa viongoz wetu wa Imani kuja katika eneo hili kutafakari masuala yao ya Imani ni tiba kubwa.”alisema na kuongeza kuwa:


“Inatia moyo kuona mwamko wa viongozi wa dini kutembelea hifadhi hii, hivyo ni chachu kwa Watanzania wengine kutembelea maeneo haya na kujionea utajiri wa rasilimali zilizopo nchini ambazo wanapaswa kujivunia na kuzilinda kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.


Mmoja wa watalii raia wa Marekani Jimbo la Calfonia, Pranav Patel aliyeambatana na familia yake kutembelea hifadhi hiyo, alisema amevutiwa na hifadhi ya Serengeti kwani ni kati ya chache bora duniani zilizowavutia kuja kujionea maajabu yake.


Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni ya tatu kwa ukubwa hapa nchini, ikitanguliwa na Mwalimu Nyerere na ya pili ikiwa ni Ruaha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI