Na Matukio Daima media
Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Lindi wameungana na Mheshimiwa Rais Samia suluhu Hassan kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwao kutoa tamko la pamoja la kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa mgombea pekee wa urais 2025 kupitia chama cha mapinduzi
Sherehe hizo zimefanyika Leo January 27, 2025 Katika viwanja vya makao Mkuu ya chama hicho huko wilalayani Lindi Mkoani Humo
Katika sherehe hizo mbunge wa Jimbo la Mchinga Mama Salma kikwete akisoma tamko Hilo kwa niaba ya jumuia hiyo aliwapongeza wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika huko jijini Dodoma kwa maamuzi Yao ya kumpitisha Rais Samia kwani alinastahili kuendelea kuwa Katika nafasi hiyo
Katibu wa umoja wa wanawake MKoa wa Lindi Bi Neema Ngongani Amesema ni faraja kwao kama jumuia kuona wanawake wanaendelea kuwatumikia wananchi na kwamba ahadi ya jumuia hiyo kwa Rais Samia ni kumpigia Kura na ushindi wa kishindo Katika Mkoa huo
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo wakatumia fursa hiyo kumpongeza Rais Samia suluhu kwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa sambamba na kupitishwa kuwa mgombea pekee wa urais kupitia chama hicho
0 Comments