Header Ads Widget

NCAA KUTANGAZA VIVUTIO VYAKE KATIKA MKUTANO WA NISHATI WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA.

Na,Jusline Marco

Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro  NCAA  imeshiriki maonesho katika Mkutano wa Nishati unaohusisha wakuu wa nchi za Afrika ikiwa ni miongoni mwa taasisi za serikali zinazoshiriki maonesho hayo,.

Wakuu wa nchi zaidi ya 25 barani Afrika, wawakilishi wa wakuu wa nchi na mashirika ya kimataifa, Tanzania ikiwa Nchi mwenyeji wamekutana kujadili na kuimarisha sekta ya nishati, jitihada za upatikanaji wa umeme, kuboresha miundombinu ya nishati, na kutafuta suluhu za changamoto zinazokwamisha maendeleo ya sekta hiyo. 

Mkutano huo ulioendelea leo  Januari  28, 2025 katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam, unalenga kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kwenye sekta ya nishati, kupitia vyanzo mbadala kama vile jua, upepo, na gesi asilia.  

NCAA inashiriki mkutano huo kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo ndani na nje ya hifadhi ya Ngorongoro na kuelezea wageni shughuli za utalii zinazofanyika ndani ya hifadhi  ikiwemo utalii wa picha,  utalii wa utamaduni na mambo kale, utalii wa miamba, Utalii wa anga kupitia Kimondo cha Mbozi, utalii wa kutembea, utalii wa kupanda milima, utalii wa puto pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo Ngorongoro.

Aidha NCAA kupitia mkutano huo inatumia fursa kutoa mualiko kwa wageni mbalimbali wanaoshiriki kutembelea eneo la Ngorongoro hususan eneo la Ndutu ambapo msimu huu ni mahsusi kwa Nyumbu wanaohama ambao wanaendelea kuzailiana kwa wingi katika eneo la Ndutu.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI