Header Ads Widget

JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MAGARI MAWILI NA MTAMBO MMOJA WA UTENGENEZAJI MIUNDOMBINU YA BARABARA.

Na,Jusline Marco;Arusha

Jumla ya shilingi bilioni 1.7 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha zimetumika kununua Malori mapya na Mtambo mpya wa kutengenezea Miundombinu ya Barabara katika kata zote za jiji la Arusha.

Akizungumza katika uzinduzi wa vifaa hivyo Meya wa jiji la Arusha uliofanyika kwenye uwanja wa Mgambo jijini Arusha, Maxmilian Iranqhe amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kuainisha barabara zote korofi ambazo zipo kwenye kata zilizo pembezoni  ili ziweze kutengenezwa.

Aidha ameishukuru halmashauri hiyo kwa kutekeleza maelekezo ya baraza la Madini kwa ununuzi wa Mtambo huo mmoja pamoja na malori mawaili na kuwataka watendaji kutumia zana hizo kama iliyokusudiwa .

Mhandisi wa halmashauri jiji la Arusha Jacob Mwakyambile akisoma taarifa fupi ya unuunuzi wa magari na mtambo huo amesema halmashauri hiyo kupitia bajeti ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/25 ilitenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 2 Kwa ajili ya ununuzi wa magari na mtanbo huo Kwa ajili ya ukarabati na utengenezaji wa Miundombinu ya Barabarq za ndani za jiji la Arusha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Arusha amesema halmashauri ya jiji la Arusha ina kata 25 na mitaa 154 ambapo katika maeneo hayo zipo barabara ndogondogo ambazo wananchi Wanapita kila siku hivyo Kupitia magari hayo na mtambo huo barabara hizo zitaenda kukarabatiwa.

Naye Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Arusha ,Willfred Soilel aliishukuru halmashauri hiyo kwa kutekeleza ilani ya ccm na kununua vifaa hivyo kwa ajili ya matengenezo ya barabara korofi na kwamba  vitasaidia kuwapunguzia kero wananchi ambapo ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Jiji kuhakikisha magari hayo na mtambo huo unatunzwa.

Uzinduzi huo umeenda sambamba na Kauli mbiu isemayo Arusha jiji la Kitalii Miundombinu Bora inayopitika wakati wote.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI