Mbunge wa Jimbo la Kilolo Justine Nyamoga (mwenye miwani katikati) akikata utepe kama ishara ya Kukabidhi gari la Wagonjwa Kituo Cha Afya Ilula wilaya ya Kilolo gari lililotolewa Wizara ya afya na usitawi wa jamii kulia kwake ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo Anna Msolla na viongozi wengine
Na Berdina Majinge Matukio Daima media
MBUNGE wa Jimbo la Kilolo Justine Nyamoga amekabidhi gari la Wagonjwa Kituo Cha Afya Ilula huku akiwataka wananchi wa kuhakikisha wanaitumia huduma ya gari la wagonjwa ili kupata huduma bora za Afya kwa wakati.
Nyamoga alisema hayo jana wakati akikabidhi gari la kubeba wagonjwa katika kituo cha afya cha Mji mdogo wa Ilula gari lililotolewa na Wizara ya afya na usitawi wa jamii na huduma ya lishe,ikiwa ni gari la tatu katika Wilaya hiyo.
Mbunge huyo alisema kuwa gari hilo litahudumia tarafa ya Mazombe na Mahenge na kuwataka wananchi kulitunza gari hilohuku akisisitiza gari hilo lifanye kazi iliyokusudiwa kwa weredi na moyo wa huruma.
“Kutokana na uwepo wa gari hili la wagonjwa hatutarajii mama mjamzito awe na changamoto ya kufika hospitali kwa ajili ya kujifungua halafu gariliwe kwenye kwenye shughuli nyingine, gari hilo limeletwa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wote bila ubaguzi lengo ni kuwafikia watu wasiokuwa na uwezo”alisema
Aidha aliwaomba watumishi na wataalamu kwa ujumla wafanye kazi kwa mujibu wa kanuni ili wananchi waweze kufurahia nchi yao pamoja na huduma zinazotolewa na serikali.
Nyamoja alisema kuwa kuna uwezekano wa moja ya vituo vya afya katika tarafa ya mazombe kupandishwa hadhi na kuwa yenye hadhi ya Wilaya ili wananchi waweze kuwa na hospitali ya Wilaya.
Pamoja na kukabidhi gari hilo katika kituo cha afya cha Ilula Nyamoga alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuendelea kumpa ushirikiano wa kutosha kuanzia sasa hadi baadaye kwa kadri wanavyoona inafaa.
“Ninawaomba wananchi mnipe ushirikiano kwa kadri ninyi mnavyoona inafaa,na mimi najua ninyi mnajua ni ipi inayofaa na kunipa ushirikiano sio dhambi kwa sababu mimi ndio Mbunge niliyeko madarakani na mimi najua tutashirikiana ili tufike pale tunapotaka kufika” alisema Nyamoga
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya cha Ilula, Raphael Haule alisema kituo kwa mwezi kinauwezo wa kuzalisha akinamama 180,na kuomba serikali iwasaidie kupata wodi la akina mama kwa sababu wagonjwa wanalala chini wodi hazitoshi.
“Tunaiomba serikali itusaidie kupata wodi la akina mama ili kuondoa adha ya wajawazito kulala vichakani, pia serikali itusaidie kupata watumishi kwani kwa sasa tunawatumishi 31 na kituo kinahitaji watumisi 59”
Kwa upande wake mwananchi mkazi wa Nyanzwa Mariam Sanga ameishukuru serikali kwa kuwaletea gari la wagongwa kwa sababu awali walikuwa wanapanda bodaboda jambo ambalo lilipelekea wengine kufia njiani kutoka na kuchelewa kufika hospitali.
“kwa sasa tunaomba serikali itusaidie kujenga uzio katika kituo cha afya kutokana na eneo hilo kutokuwa salama pia tunaomba serikali itujengee wodi la akina mama wanaojisubiria kujifungua
0 Comments