Na Zuhura Zukhery, Matukio daima, Iringa
MWENYEKITI wa umoja wa Vijana wa Chama Cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Agrey Tonga awataka Vijana kuwa wazalendo katika Taifa kwa kukupambania ushindi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na CCM kwenye Uchaguzi mkuu mwaka huu.
Kuwa vijana mkoani Iringa wanajukumu la kuwa wazalendo na kuishi kwa muongozo wa chama chao ili kuendelea kuijenga CCM iliyo imara kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa.
Tonga alitoa Kauli hizo Mbele ya mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Salim Abri Asas wakati akitoa salamu za UVCCM katika uzinduzi wa Sherehe za miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM iliyofanyika wilaya ya kilolo kimkoa kuwa ni wajibu wa kila kiongozi wa UVCCM kumuandaa kijana ili kuwa mrithi wa uongozi baadae ambaye atasimamia muongozo wa chama cha mapinduzi.
“Rai yangu kwa wanachama wa UVCCM na viongozi wote kuhakikisha wanawaandaa vijana kuwa viongozi wa wazalendo wa badae na tuwafanye viongozi hao kuwa sauti ya urithi wa CCM vizazi na vizazi na haya yote hayatawezekana kama sisi tutakuwa hatujawaandaa vijana hawa kuwa wazalendo kwa chama chao”alisema Tongwa.
Alisema kuwa kama UVCCM itaweka misingi imara kwa jumuiya za vijana ni vigumu kuipata jumuiya ya UWT au jumuiya ya wazazi iliyobora kutokana na mizizi ya jumuiya na chama kwa ujumla huanzia kwa vijana.
Aidha Tonga alisema kuwa katika kuadhimisha miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM kila mwanaccm aweke mikakati imara ya kuhakikisha ushindi wa kiti cha urais kwa Dkt Samia Suluhu Hassan unakuwa ni wa kishindo kwa mkoa wa Iringa.
Alisema zawadi pekee kwa CCM kutimiza miaka 48 yakuanzishwa kwake ni kuhakikisha katika uchaguzi mkuu kura za Rais, wabunge, na madiwani zinakuwa za kutosha kama ilivyokuwa katika chaguzi za serikali za mitaa.
“wakati wana CCM tunafurahia miaka hii 48 ya kunzishwa kwa CCM niwaombe wanachama wenzangu nendeni mkakipambanie chama kawaelezeni wananchi utekelezaji wa ilani ya CCM uliyofanywa kwa miaka yote hiyo, haya yaliyofanywa na CCM yanapaswa kupongezwa na wananchi wote bila kujali itikadi ya vyama vyao kwakuwa chama hiki jamani kimekuwa kikisimamia serikali kwa amani bila kuwa na migogoro au viashiria vya uvunjifu wa amani”alisema Tonga
Akizungumzia mchango wa MNEC Asas alisema kuwa MNEC huyo amekuwa na mchango mkubwa wa kukijenga chama hicho ndani na nje ya mkoa wa Iringa kwa kuhakikisha chama hakitetereki wala hakijigawi kimafungu.
Tonga alisema kuwa vijana wanapaswa kumuunga mkono MNEC Asas kutokana na mchango mkubwa alionao katika chama hicho kuanzia ngazi ya mashina hadi mkoani.
“Tunazima zote tunawasha Kijani, ndugu zangu wanaccm tusema kweli huwezi kuitaja CCM Iringa bila kumtaja MNEC Asas hakuna wilaya iliyokuwa imeanzisha mradi bila MNEC Asas kutia mkono wake hivyo amekuwa na mchango mzuri sana katika chama chetu tumpe ushirikiano tusimuangushe hasa sisi vijana ndio nguzo imara ya chama chetu, katika miaka hii 48 tutembee kifua mbele kuyasemea mazuri yanayofanywa na serikali ya ccm inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan”alisema Tonga.
0 Comments