Header Ads Widget

RC MWASSA AFIKA TARAFA YA KATERERO KUKAGUA UKARABATI BANDARI YA KEMONDO ULIOGHARIMU BILIONI 20


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa leo Jumanne Januari 28, 2025 amefanya ziara ya aina yake kwenye Tarafa ya Katerero kwa kutembelea kukagua ukarabati wa Bandari ya Kemondo uliogharimu takribani Bilioni 20 huku kazi ikiwa imekamilika kwa asilimia 100 chini ya Mkandarasi Kampuni ya Kichina China Railway Major Bridge Engineering Limited. RC Mwassa na viongozi aliombatana nao walipokelewa na Kaimu Mkuu wa Bandari Bw. David Nicodem na kutembezwa kukagua maeneo yote ya bandari.


Akipokea taarifa ya ukarabati wa Bandari hiyo, RC Mwassa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa Bilioni 20 alizoleta Bandari ya Kemondo kuikarabati kwa kuongeza gati kubwa zenye uwezo wa kupokea meli kubwa zaidi, ujenzi Jengo la Kisasa la abiria na Jengo la mizigo.


RC Mwassa aliambatana na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto aliyeambatana pia na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku, Mtendaji wa Kata ya Kemondo Ndugu Cyriacus Sosthenes na viongozi wengine.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI