Na Matukio Daima media
UAMUZI mzuri wa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuagiza fedha za zilizotengwa kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru kuelekezwa kwenye huduma za kijamii badala ya gwaride la Kitaifa wapongezwa.
Mwamasishaji wa Vijana na maendeleo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Shalom Robert ameibuka na kupongeza hatua hii akisema ni mfano bora wa uongozi wa kipekee unaojali maendeleo ya watu.
Shalom ambae kitaaluma ni Mwanahabari anasema kuwa hatua ya Rais Samia kuamua kwamba maadhimisho haya yafanyike katika ngazi ya mikoa, yakilenga shughuli za kijamii kama usafi wa mazingira, upandaji miti, na midahalo ya maendeleo ni jambo lenye tija na litafanya Kila mmoja kuadhimisha Miaka 63 ya Uhuru .
Shalom anasema uamuzi huu unaonyesha kipaumbele cha serikali katika kuimarisha ustawi wa wananchi kwa kutumia rasilimali kwa njia endelevu.
Kuwa badala ya kutumia fedha kwa gwaride na shughuli za kitaifa zisizo na athari za moja kwa moja kwa wananchi, fedha hizo zitatumika kuboresha sekta za afya, mazingira, na ustawi wa jamii
“Uamuzi huu ni ishara dhahiri ya uongozi unaotanguliza maslahi ya wananchi. Ni hatua inayoonyesha kujali mahitaji ya msingi ya jamii, hasa katika kipindi ambapo changamoto za kiuchumi zinahitaji busara ya matumizi ya rasilimali za taifa,” amesema Shalom.
Shalom ambae hivi karibuni wazee wa Kijijini kwao Kilosa Kata ya Ihanu Wilaya ya Mufindi walimpa heshima ya kichifu alisema kuwa kauli mbiu ya maadhimisho hayo, "Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo Yetu," inaakisi kwa dhati maudhui ya maamuzi ya Rais Samia.
Shalom alisema kuwa kushirikisha wananchi katika shughuli hizi ni njia bora ya kuimarisha uzalendo na kujenga mshikamano wa kitaifa.
Hivyo aliwataka Vijana wa wilaya ya Mufindi na Taifa kwa ujumla kuunga mkono uamuzi huo mzuri wa Rais Dkt Samia kwa Kila mmoja kushiriki shughuli ya kijamii katika eneo lake.
Kuwa haitapendeza kuona Vijana wakiwaachia wazee Pekee kushiriki maadhimisho hayo Kwa kufanya kazi huku Wao wakibaki vijiweni kuwa Watazamaji .
Kwa mujibu wa maelekezo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, shughuli za kijamii zitaendeshwa kwa ushirikiano wa karibu kati ya mikoa, wilaya, na wananchi. Hii ni fursa ya kuonyesha mshikamano na kutafakari kuhusu mafanikio yaliyopatikana tangu kupata uhuru mwaka 1961.
Shalom anasema, “Kwa kushirikiana katika shughuli hizi, wananchi wanapata nafasi ya kuenzi uhuru wao huku wakihamasishwa kuchangia maendeleo ya jamii kwa vitendo. Huu ni uongozi wa mfano unaothamini ushirikiano wa jamii nzima.”
Alisema Fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe za kitaifa sasa zitasaidia kuboresha huduma za kijamii. Hii ni pamoja na miradi ya afya, msaada kwa kambi za wazee na watu wenye mahitaji maalum, pamoja na upandaji miti unaochangia kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Mwamasishaji huyo wa Vijana katika maendeleo Shalom anaona kuwa hatua hii itakuwa na athari kubwa kwa maisha ya watu wa kawaida, hasa wale wanaoishi katika mazingira yenye changamoto za kijamii na kiuchumi.
“Kupanda miti sio tu kunasaidia mazingira bali pia kunaimarisha hali ya hewa na uzalishaji wa chakula kwa jamii zetu.
Kuwekeza kwenye hospitali na kambi za wazee ni ishara ya uwajibikaji wa serikali kwa makundi maalum katika jamii,” anasema.
Hata hivyo Shalom ameelezea jinsi maamuzi ya Rais Samia yanavyoakisi uongozi wa kipekee unaozingatia misingi ya maendeleo endelevu.
Anasema, "Rais Samia anaendelea kuthibitisha kuwa uongozi wake sio wa kawaida.
Kuwa ni wa kimkakati, wenye maono na unaojali watu wa hali ya chini uamuzi huu ni ushahidi kuwa Tanzania iko katika mikono salama."
Kwa kuelekeza rasilimali kwenye maeneo yenye tija, Rais Samia anaonyesha kuwa sherehe za uhuru hazihitaji kuwa za kifahari ili kuenzi historia ya nchi.
Kuwa badala yake zinaweza kuwa jukwaa la kuimarisha maisha ya wananchi na kuweka msingi wa maendeleo endelevu.
Hata hivyo Shalom anaonya kuwa mafanikio ya maadhimisho haya yatategemea utekelezaji bora wa maelekezo haya ngazi ya mikoa na wilaya.
Ushirikiano wa karibu kati ya viongozi wa serikali za mitaa na wananchi ni muhimu kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakuwa ya kudumu na yenye manufaa ya kweli.
"Tunaweza kuangalia jinsi ya kutumia rasilimali zetu kwa ufanisi zaidi kwa kuiga mfano huu. Sherehe za kitaifa zinaweza kuwa kichocheo cha maendeleo badala ya matumizi makubwa yasiyo na tija."
Kwa uamuzi huu wa kipekee, Rais Samia ameonyesha kuwa sherehe za uhuru zinaweza kuwa zaidi ya kumbukumbu ya kihistoria.
Shalom Robert anasema kuwa "Uongozi wa Rais Samia ni wa kimkakati na unaotanguliza ustawi wa jamii.
Kuwa hatua hii ni somo kwa viongozi wengine wa Afrika na duniani kote kuhusu umuhimu wa kutilia mkazo maendeleo ya watu badala ya maonyesho ya kifahari."
Ikumbukwe kuwa miaka 63 ya uhuru wa Tanzania Bara, hatua ya kuelekeza fedha za sherehe kwenye maendeleo ya jamii ni ukumbusho wa thamani ya uhuru – sio tu kuwa huru kisiasa, bali pia kiuchumi na kijamii.
Kuwa Rais Samia ameonyesha kuwa uhuru wa kweli ni ule unaoleta mabadiliko chanya kwa maisha ya wananchi wake.
Shalom Robert ni kijana mwenye umri mdogo ambae umoja wa Wazee wa Mila za asili kutoka Kijiji Cha Kilosa Kata ya Ihanu Wilaya ya Mufindi, walimpatia heshima ya asili kwa kumuita Chifu KEKOVANGU jina linalomaanisha "Mkombozi wetu".
0 Comments