Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe Mhe.Erasto Mpete amewataka wananchi kuwa makini wakati wa sherehe za Krismas na Mwaka mpya ikiwemo kuacha ulinzi majumbani wakati wa mikesha ili kuepusha wizi na matukio mengine ya kihalifu.
Mpete ametoa wito huo mbele ya vyombo vya habari wakati akitoa salaam za siku kuu za mwisho wa Mwaka na kwamba katika kipindi hiki matukio mengi ya kihalifu hutendeki na hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini.
Aidha amewataka wananchi kuwa makini na kunywa kiasi pindi wanapokuwa sehemu za starehe kwani kuzidisha kileo Kuna weza kusababisha ugomvi unaoweza kusababisha majanga kwa mnywaji mwenyewe au watu wengine.
Kwa upande wa madereva amewataka kuwa makini wanapoendesha vyombo vya moto na kutotumia kilevi kwani ajali nyingi hutokea katika kipindi Cha siku kuu hizo.
Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kukumbuka mahitaji ya shule kwa watoto hapo januari wakati shule zikifunguliwa badala ya kutumia fedha zote kwenye siku kuu za Krismas na Mwaka mpya.
0 Comments