Header Ads Widget

"DINI, SIASA VISIWAGOMBANISHE WATANZANIA"- DKT. MPANGO





Na Fadhili Abdallah,Kigoma


MAKAMU wa Rais Dk.Philip Mpango ameongoza Watanzania katika mazishi ya Margret Ntibhayizi Mama yake Mzazi Mkuu wa mkoa Iringa Peter Serukamba huku akiwaonya watanzania kuwa tofauti za kiimani za dini zao na tofauti za kiitikadi za vyama vyao vya siasa isiwe kigezo cha kuwafanya wafarakane na kushindwa kusaidiana kwenye shughuli za kijamii.


 Katika mazishi yaliyofanyika katika mji mdogo wa Mwandiga wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma Makamu huyo wa Raisi alisema kuwa Watanzania ni ndugu na kwa umoja wao wanapaswa kupandana na kushirikiana kwa kila jambo linalotokea kwa umoja na mshikamano wao jqmbo ambalo ni muhimu katika maisha ya kila siku ya Mwanadamu.



Katika hilo alisema kuwa misingi ya dini zote zinahimiza umoja,Amani na mshikamano sambamba na kupendana na kwamba dini zinahimiza kila binadamu kumpenda mwenzake bila kuwepo kwa ubaguzi wa aina yeyote.


Akizungumzia suala la kuporomoka kwa maadili Makamu huyo wa Raisi alisema watu wengi kuacha kuzingatia misingi ya dini zao ndiyo kumesababisha kuendelea kwa vitendo viovu ikiwemo ukatili, ubakaji na ujambazi hivyo kuhimiza Watanzania kupiga vita vitendo hivyo kwa kuzingatia misingi ya dini zao.




Akisoma wasifu wa Marehemu na kuwasilisha salamu za familia Mkuu wa mkoa Iringa,Peter Serukamba alisema kuwa mama yake Mzazi, Margaret Ntibhayizi amefariki akiwa na miaka 83 ambapo amecha mtoto mmoja tu ambaye ni yeye.


Serukamba alisema kuwa mama yake amefariki akiwa mcha Mungu ambaye muda wote alizingatia misingi ya dini na kwamba hata alipokuwa anazidiwa aliomba kuitiwa viongozi wa dini kumuombea.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI