Na Moses Ng'wat, Mbozi.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe kimebainiasha kuwa, hakitasita kuwaondoa kwenye nafasi zao Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa, wakiwemo wajumbe wa Serikali za Vijiji watakaobainika kuwa chanzo cha migogoro kwenye maeneo Yao ya uongozi.
Hayo yamebainishwa Desemba 23, 2024 na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Songwe Silvester Mbanga wakati akizungumza kwenye mafunzo ya siku moja ya matokeo ya sensa ya watu na makazi yaliyoandaliwa na mbunge wa jimbo la Vwawa, Japhet Hasunga kwa kushirikana na ofisi ya mtwakumu mkuu wa serikali(NBS).
Mbanga amesema, migogoro mingi kwenye vijiji na vitongoji husababishwa na viongozi ambao wamekuwa wakitumia madaraka vibaya tofauti na matakwa ya wananchi ambao wamewachagua.
"Ninyi viongozi mliochaguliwa mnapaswa kwenda kuwatumikia wananchi waliowaxhagua, hatutaki kusikia mnakuwa chanzo cha migogoro, kunawakati mnasabibisha migogoro ya ndoa kwa kutongoza wake za watu na waume za watu kwa kutumia nafasi zenu...sasa tukikubaini kama chama hatutawaacha salama tutawaondoa na kuitisha uchaguzi mdogo," amesisitiza Mbanga
Amewasisitiza viongozi hao kuzingatia mafunzo waliyoyapata yakawawe chachu ya mfano kubuni vipaumbele vya maendeleo yanayohitajika kwa wananchi kulingana na idadi ya wananchi iliyopatikana kipindi Cha sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Vwawa, Japheti Hasunga, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwasaidia kuwajengea uwezo viongozi hawa ambao wamekuwa wakilalamikiwa kusababisha migogoro kwenye maeneo yao ikiwepo ya ardhi
Hasunga amesema mafunzo hayo yatawasaidia kujuwa umuhimu wa takwimu ya sensa ya watu na makazi kwa kuibua vipaumbele vya maendeleo sambamba na kupata mafunzo ya kusuluhisha migogoro na kuwa faraja kwa wananchi.
"Viongozi wengi wa vijiji na mitaa mnatumia madaraka yenu vibaya kuuza maeneo hovyo kwa kutumia ,hivyo mafunzo yatakuwa mwongozo kwenu kwenye uongozi wa miaka mitano tangu mmechaguliwa kwenye uongozi wa serikali za mitaa Novemba 27,2024," amesema Hasunga.
Kwa upande wake mgeni rasmi wa mafunzo hayo ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Radiwelo Mwampashi, amewataka viongozi wa vijiji na vitongoji kutumia mafunzo hayo kwenda kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na kutatua changamoto za wananchi
Naye, Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Benedicti Mgambi, amesema kwa mujibu wa Takwimu ya sensa ya watu na makazi mkoa wa Songwe unajumla ya wakazi milioni 1.34 ,huku wilaya ya Mbozi ikiwa na zaidi ya wananchi laki 5.1 sambamba na mkoa kuwa na asilimia 50.7 ya watoto chini ya miaka 18.
Mgambi amesema wilaya ya Momba Ina watu tegemezi 115 Kila watumia wenye uwezo wa kufanya kazi na mji wa Tunduma ndo halmashauri yenye idadi ndogo ya watu 77 kwa kila watumia wenye uwezo wa kufanya kazi.
"Tumieni matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa maendeleo ya uchumi kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, kata, wilaya ,Mkoa na taifa kwani ndio msaada wa kutengeneza mipango ya maendeleo kulingana na idadi ya wananchi kwenye maeneo husika" amesema Mgambi.
0 Comments