Header Ads Widget

MILIONI 420 ZA MBUNGE MWANYIKA ZATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA NJOMBE MJINI

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakati mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Akitumia zaidi ya shilingi milioni 400 toka mfukoni mwake kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo wananchi wa jimbo hilo wamepongeza jitihada hizo na kutaka kusaidiwa kutatua kero za barabara zinazowakwamisha kwenye baadhi ya maeneo hivi sasa.

Wakazi hao wametoa ombi hilo baada ya mbunge huyo kusoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake na kwamba kwenye maeneo yaliyokwama wanaomba yashughulikiwe kwani bado wana imani naye.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika huko Hagafilo mjini Njombe wakati akiwasilisha taarifa hiyo Mbunge Deo Mwanyika amewataka wananchi kuvuta subira juu ya miundombinu ya barabara kwani serikali imeshatenga  fedha zaidi ya shilingi bilioni 100 za kutatua changamoto hizo.

Halima Mamuya ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njomba ambaye alikuwa mgeni wa Heshima katika usomaji wa Utekelezaji wa Ilani katika Jimbo la Njombe Mjini Yeye anawataka wajumbe wote walioshiriki na kusikiliza Taarifa hiyo kwenda kuwaeleza wananchi mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minne ya Mbunge Mwanyika.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI