Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MAMLAKA ya mapato nchini (TRA) imesema kuwa vikao na ziara wanazofanya na kukutana na wafanyabiashara kuzungumzia changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika ulipaji kodi umechochea ulipaji kodi kwa hiari na kuifanya mamlaka hiyo kuvuka malengo ya ukusanyaji.
Kamishna wa upelelezi wa kodi (TRA), Hashim Ngoda alisema hayo walipofanyaza ziara mkoani Kigoma kuwatembelea, kuzungumza na kutoa zawadi kwa baadhi ya wafanyabiashara kutambua mchango wao na kuwa mabalozi kwa wengine katika suala zima ulipaji kodi kwa hiari.
Ngoda akimwakilisha Kamshna Mkuu wa TRA, Yusuf Mwenda alisema kuwa tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wakifika kwenye maduka na kuzungumza nao lakini wakati mwingine kufunga maduka hali iliyokuwa inafanya wafanyabiashara wengi kufunga maduka na kukimbia hali ambayo ni tofauti na sasa.
Kamishna huyo wa upelelezi alisema kuwa vikao, mikutano na ziara hizo zimekuwa zikifurahiwa na wafanyabiashara na vimekuwa na matunda makubwa katika kukabiliana na uingizaji wa bidhaa za magendo na hali hiyo imefanya kuwepo kwa ongezeko kubwa la makusanyo hivyo kufikia na kuvuka lengo.
Akizungumza baada ya kupokea zawadi kutoka kwa uongozi wa TRA Mkurugenzi wa kampuni ya Falcon Marine, Mbaraka Mussa alisema kuwa ziara hizo zimekuwa Faraja kubwa kwao kuona namna TRA inavyowajali na kushughulikia matatizo yao ya kikodi.
Naye Mfanyabiashara wa duka la jumla soko kuu la mjini Kigoma, Kilahumba Kivumo aalisema kuwa amejisikia Faraja sana TRA kumtembelea na kumpa zawadi na kwamba hali hiyo inaongeza motisha kwao katika kusimamia ulipaji kodi kwa hiari.
Mwisho.
0 Comments