Na,Jusline Marco;Arusha
Katika Mkutano wa pili wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika uliofanyika Disemba 2 na kumalizika Disemba 5 jijini Arusha wadau mbalimbali wameweza kukutana katika maonesho yaliyoambana na mkutano huo kwa lengo la kutoa elimu na huduma kwa wadau wa sekta ya Uhasibu na Ukaguzi wa ndani.
Mkuu wa Masoko na Mauzo kutoka APC Hotel and Conference Centre iliyopo Bunju Mbweni jijini Dar es salaam, Michael Mwakifuna amesema ushiriki wao kwenye maonesho hayo katika mkutano huo ni ili kuitangaza hoteli hiyo kwa wadau mbalimbali nchini na nje ya nchi.
Michael amesema Hotel hiyo ambayo inamilokiwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania NBAA, ina miaka saba tangu kuanzishwa kwake, ina uwezo wa kuchukuwa idadi ya watu tofauti na kumbi zaidi ya kumi ambayo pia iko katika eneo lenye ukubwa wa hekari 13 iliyojumuisha viwanja mbalimbali vya michezo.
Amesema kuwa lengo kubwa la kuanzisha hoteli hiyo ni kusaidia katika shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na NBAA pamoja na sekta tofautitofauti ili kuweza kukuza maendeleo ya nchi.
Pamoja na hayo amesema hatua hiyo inaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutangaza Utalii wa Mikutano na Biashara kupitia sekta ya Utalii hivyo ujio wao jijini Arusha utawawezesha katika uungaji mkono kauli hiyo na kuingia kwenye mnyororo wa thamani.
0 Comments