Header Ads Widget

JESHI LA POLISI MKOANI MOROGORO LIMEIMARISHA ULINZI WAKATI WA KUELEKEA MWISHO WA MWAKA


 JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limeimarisha ulinzi na usalama wakati huu wa kuelekea mwisho wa mwaka ambapo operesheni na doria katika maeneo mbalimbali zimeimarishwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mtama amesema katika operesheni zinazoendelea, wamefanikiwa kuwakamata madereva 70 kwa makosa hatarishi ya matumizi mabaya ya barabara.

Akasema kati ya madereva hao, 32 wameamuriwa na Jeshi hilo kurudi shuleni kwaajili ya kupigwa msasa kwenye masuala ya Sheria za usalama barabarani na matumizi sahihi ya barabara na madereva 38 waliamdikiwa faini.

Aidha amesema madereva wengine 19 wamefungiwa leseni zao na kati yao tisa ni kutokana na kuendesha wakiwa katika Hali ya ulevi, saba kwa makosa ya mwendo Kasi na watatu wamefungiwa moaka kesi zao zitakapoisha mahakamani kwa makosa ya kuendesha kwa uzembe na kusababisha ajali.

Kamanda huyo wa Polisi akawaondoa hofu wananchi katika kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka kuwa wamejipanga vizuri kukabiliana n vitendo vyote vya uhalif na kuonya atakayethubutu kufanya uhalifu, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Akatoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu na madereva kuheshimu Sheria za barabarani Ili kuokoa maisha ya watu na Mali zao wakiwemo abiria na watumiaji wengine wa barabara.

Mkama pia akawaonya madereva kuacha kunywa pombe na kuendesha magari kwasababu ni hatari kwa usalama wai, abiria na watumiaji wengine wa barabara.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI