Na. Matukio Daima App, Kilosa.
WIZARA ya Katiba na Sheria inatarajia kufanya operesheni maalum wilayani Kilosa Mkoani Morogoro ya kutatua migogoro papo kwa papo kwa kishirikisha wataalam wa sekta mbalimbali sambamba na mahakama inayotembea kutatua migogoro iyakayosindwa usuluhishi.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Damas Ndumbaro alisema hayo Katika Kata ya Magomeni wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wakati akizindua kampeni ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia Legal Aid wilayani humo na kuahidi kuongoza opresheni hiyo.
Akasema operesheni hiyo itakayoanza baada ya siku kumi za Kampeni ya msaada wa Kisheria kwa Mkoa wa Morogoro zinapenga kutatua changamoto zinazoikavbili wilaya ya Kilosa ambayo imeshika kasi katika migogoro ya Ardhi na Ile ya wakulima na wafugaji.
Akawataka ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kilosa na Ofisi ya mwendesha Mashtaka wa Serikali kuwa tayari kwa zoezi hilo ikiwemo kuwaandaa
walalamikaji, walalamikiwa na mashahidi katika maeneo yenye migogoro ili wasikilize na kuamua papo hapo na ambaye hataridhika na maamuzi aweze kusigea penye mahakama inayotembea.
"Nimepokea Maombi na ushaurii ulliotolewa na viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Kilosa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Prof Paramagamba Kabudi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.Adam Malima na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Bw.Shaka Hamdu Shaka na tufanaya opreshwni hii zikimaliza siku 10 za Kampeni, na Mimi ndiye nitaongoza"Alisisitiza.
Akasema maelekezo ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha elimu ya msaada wa Kisheria inawafikia wananchi wengi hasa wanyonge na wasio na uwezo pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili bila gharama katika Kampeni hii ya msaada wa kisheria ya Mama Samia"Alisema Waziri Ndumbaro.
Waziri huyo mwenye Dhamana ya Katiba na Sheria alisema migogoro mingi kwenye jamii inachangiwa na watu kutojua haki na Wajibu wao au kutojua Sheria lakini kupitia elimu ya msaada wa kisheria wengi watajua hatua za kufanya na kuondoa au kupunguza migogoro iliyopo kwani unachangia uvunjifu wa amani na kukosekana maendeleo ya watu wa maeneo husika.
"Wananchi wengi hawafahamu elimu ya Sheria, na hii inasababisha changamoto mbalimbali kuendelea kuonekana zipo, lakini tukumbuke ili maendeleo yawepo katika eneo lolote ni Lazima Amani iwepo, ndio maana kampeni hii inalenga kuelimisha watu ili kupunguza ama kumaliza migogoro ya Kisheria inayoibuka kwenye jamii "Alisisitiza Waziri
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Mochezo Prof Paramagamba Kabudi alisema tayari Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Waziri wake Mhe Dkt.Ashatu Kijaji imetangza wilaya ya Kilosa kuwa Kanda maalum ya kushughulikia matatizo ya wakulima na wafugaji kutokana na wilaya hiyo kuongoza kwa migogoro ya Ardhi na ya wakulima na wafugaji.
Aidha akasema Mawaziri mbalimbali wamekusudia kwenda wilayani Kilosa ili kushughulikia changamoto zilizopo akiwemo Waziri wa Kilimo, Waziri wa Ardhi na Waziri wa Mifugo .
Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.Adam Malima, alisema simu nyingi anazopokea za malalamiko wilaya inayoongoza ni Kilosa ikifuatiwa na Kilombero.
"Wakati mwingine migogoro mingi ni kutokana watu kukosa elimu ya Sheria na kushindwa kujua tatizo lake linapaswa kutatuliwa na Mamlaka zipi kwani mengine ni masuala ya kisheria"Alisema Malima na kukiri wilaya ya Kilosa ni kubwa ikiwa na kilometa za mraba12,000 na wanahitaji zaidi huduma hizo za msaada wa kisheria kwa upana wake.
Mapema mkuu wa wilaya ya Kilosa Bw Shaka Hamdu Shaka licha ya jitihada zinazofanywa na Serikali kwa wananchi wa Kilosa ikiwemo miradi katika sekta mbalimbali ya thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 63 ikiwemo sekta za afya, elimu, Uchumi na kijamii akasema migogoro ya Ardhi na Ile ya wakulima na wafugaji bado imeshika kasi wilayani hump.
Hata hivyo akasema uwezo mdogo wa wananchi kushindwa kuhimili gharama za maisha kumefanya wengi kushindwa kupata hakii stahili na kwamba asilimia zaidi ya 85 ya migogoro watakayopokea wataalam katika Kampeni hiyo itahusa Ardhi na migogoro ya wakulima na wafugaji.
"Wilaya ya Kilosa ni kubwa sana ili wananchi wengi zaidi wa vvijijini wafikiwe wenye uhitaji, wafikiwe Tunaomba tuongezewe muda na vijiji na Kata nyingi zaidi katika kampeni hii"Alisema Mkuu huyo wa wilaya.
Shaka pia akaiomba wizara ya Katiba kuongeza wanasheria zaidi katika ofisi ya Mashtaka Wilayani humo kwani kesi zilizopo ni nyingi na zinahitaji utatuzi ambapo kwa sasa kuna kesi karibu 260 zilikuwa bado kwenye utaratibu wa kwenda mahakamai
0 Comments