Header Ads Widget

TAHADHALI YATOLEWA KUELEKEA SIKUKUU ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA

 

.Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa amewatahadhalisha Wananchi Mkoani Kagera kujiepusha na na matumizi ya vilevi haswa madereva wawapo barabarani ili kuepuka ajali ambazo zinapoteza uhai wa Watanzania.

Mwassa ametoa Kauli hiyo, wakati akiongea na waandishi wa habari katika Ofisi za Mkoa huo,Amesema kuwa ulevi kwa asilimia kubwa unasababisha ajali hivyo watumiaji wa vyombo vya moto wahakikishe waendeshe kwa umakini ili waepuke ajali zinazoweza kujitokeza.

"Tunaposherehekea siku kuu hizi za Christmas na Mwaka mpya tujiepushe na yote yanayoweza kutugharimu pia wazazi tuwaangalie watoto wasitembee wenyewe barabarani kwani ajali ni nyingi lakini msiwaruhusu kwenda fukwe za bahari bila uangalifu" alisema Mwassa.

Alisema kuwa Mkoa ulimpoteza mtoto hivi karibuni baada ya kuzama ziwani hivyo sehemu zote za hatari wasipelekwe watoto kucheza,Aidha aliongeza kuwa katika siku kuu hizo ni vyema watoto wakapelekwa katika maeneo yanayotambuliwa kwa michezo yao, piaMkuu huyo  alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi kutowapeleka watoto katika maeneo ya baa ili kulinda ustawi na makuzi ya mtoto.

Hata hivyo alieleza kusikitishwa na ajali iliyotokea Wilayani Biharamulo Mkoani humo iliyosababisha watu 11 kufariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa ikiwa siku za hivi karibuni pia kumetokea ajali mbaya katika Wilaya ya Karagwe na kusababisha vifo na majeruhi ambapo pia aliwapa pole Watanzania na wanakagera kutokana na majonzi hayo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI