Header Ads Widget

SMAUJATA TAIFA YATANGAZA MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI KATIKA JAMII.

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Watanzania wametakiwa kuwa na moyo wa ustahimilivu pindi wanapokutwa na changamoto mbalimbali badala ya kuchukua maamuzi yanayoweza kuigharimu jamii katika maisha.

Katika mkutano na wanahabari mkoani Njombe mkurugenzi wa uenezi vijana na michezo Wa Shujaa wa Maendeleo na ustawi wa jamii Taifa  SMAUJATA  Ndugu Johnson Mgimba amesema kujichukulia hatua kwa hasira pindi unapokutwa na tatizo kumekuwa kukisababisha kutokea kwa matukio ya ukatili jambo ambalo linapaswa kupingwa na kila mwananchi.

Mgimba amesema ukatili unaotendeka katika jamii yakiwemo mauaji ya kikatili,ubakaji,ulawiti pamoja na Utekaji hautokani na masuala ya kisiasa pekee Bali ni roho za kikatili zinazopaswa kupingwa kwa nguvu zote kwani serikali haiwezi kufanya uchunguzi Hadi kwenye roho za watu.

Siku chache zilizopita mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka wakati akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa kujadili hali ya ulinzi na usalama ya mkoa aliapa kupambana na matukio ya kikatili na mauaji yanayoendelea kuripotiwa katika Maendeleo mbalimbali.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI