Header Ads Widget

WAZIRI DKT CHANA AZINDUA UTALII WA PUTO HIFADHI YA RUAHA ATAJA MAFANIKIO LUKUKI

 



NA MATUKIO DAIMA MEDIA IRINGA 


WAZIRI  wa Maliasili na Utalii Balozi, Dkt. Pindi Chana amehitimisha Kilele Cha maadhimidho ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa kuzindua  utalii wa puto.


Uzinduzi huo umefanyika Leo katika eneo la Korongo View ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha Mkoani Iringa.


Akizungumza baada ya uzinduzi huo Dkt  Chana alisema mafanikio hayo ni kutokana na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii.


"Tunamshukuru Rais Samia kwa kuionesha dunia vivutio vya utalii vya Tanzania ambapo mpaka sasa watalii wameongezeka na kufikia milioni 1.8 na mapato ya Taifa tunachangia asilimia 17% na fedha za kigeni takribani dola za kimarekani Bilioni 3.6.


Kuhusu maboresho ya Miundombinu katika Hifadhi ya Taifa Ruaha Dkt Chana alisema kuwa hadi sasa kuna barabara ya Iringa- Msembe yenye urefu wa kilomita 104 ambayo inaenda kujengwa.





Alisema katika Hifadhi ya Taifa Ruaha kutakuwa na uwanja wa ndege sambamba na kutumia uwanja wa ndege wa Nduli uliopo Mkoa wa Iringa ambao unaendelea kukarabatiwa


Aidha alisema kuwa kwa miaka 3 kumekuwa na mabadiliko makubwa ya sekta ya utalii na Serikali inazidi kuboresha maeneo mengi ya Utalii huku akihamasisha wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika hifadhi hiyo ya Ruaha .


waziri Dkt Chana alisema Wizara ya Maliasili na utalii imekuwa ikifanya kazi kubwa kusimamia Hifadhi Zote 21 nchini kuona zinaendelea kuwa tegemeo kubwa kwa Taifa.


Alisema kuwa Wizara hiyo ipo kutekeleza 4R za Rais Dkt Samia hivyo ndio maana Wizara hiyo hailali inaendelea kupiga kazi .


Akielezea kuhusu Hifadhi ya Ruaha alisema kuwa Hifadhi ni Moja kati ya Hifadhi kongwe nchini hivyo Mafanikio makubwa yameonekana kupitia Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Hifadhi hiyo.



Waziri Dkt Pindi alisema kuwa Hifadhi za Taifa zinatoa mchango mkubwa katika Taifa kwenye nyaja mbali mbali na kuwa Pato la Taifa limekuwa likichangia kwa kiasi Kikubwa kupitia sekta hiyo.


Hata hivyo alisema kupitia jitihada za Rais Dkt Samia kutangaza utalii maendeleo makubwa yameendelea Kuwepo.


"Maendeleo haya yote yametokana na utulivu na amani iliyopo nchini kutokana na misingi Bora ya serikali chini ya Rais Dkt Samia"


Hata hivyo akizungumza kwa niaba ya Wahifadhi wastaafu wa Hifadhi hiyo Loriviole Moirana pamoja na Kupongeza jitihada kubwa za kuboresha Hifadhi hiyo bado waliitaka serikali kuendelea kuikumbuka Hifadhi hiyo kwa Kutenga fedha za uendeshaji na kuzituma kwa wakati.


Ili ziweze kusaidia kuendesha Hifadhi hiyo pamoja na kuomba fedha kutumwa kwa wakati Bado waliomba Hifadhi hiyo kuwe na ndege zaidi ili kusaidia Kupambana na matukio ya ujangili pamoja na uendeshaji wa Hifadhi hiyo.


"Serikali iwe mstali wa Mbele katika kuwezesha wafanyakazi wake kwani hili ni jeshi hivyo lazima serikali iwapo ushirikiano hili ni jeshi unamwambia mtu alinde mipaka ya Hifadhi bila ushirikiano wa serikali ni kazi Ngumu sana "



Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Peter Serukamba alisema kuwa Hifadhi ya Ruaha ni Hifadhi muhimu sana ambayo imefanya mkoa kuendelea kutangazika kupitia utalii.


Mkuu huyo wa mkoa alipongeza wadau mbali mbali wa utalii ikiwemo kampuni ya Foxes ambao ndio waasisi wa utalii katika Hifadhi hiyo .


Hata hivyo alisema kupitia jitihada za wadau wa Utalii Hifadhi hiyo imepiga hatua kwa kuanzisha utalii wa Puto.


Pia alisema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia imeendelea kufanya jitihada kubwa kwa kufungua utalii kwa kupitia filam ya The Royal Tour pamoja na Mradi mkubwa wa Regrow ambao unajenga viwanja vya ndege viwili kiwanja Cha Iringa na kiwanja Cha Msembe pamoja na ujenzi wa lami kilomita 104 .


Kuwa ujenzi wa barabara hiyo na viwanja vya ndege viwili ni wazi Kasi ya utalii itakuwa zaidi ndani ya Hifadhi ya Ruaha na kuwataka wadau wa sekta ya utalii kuendelea kujitokeza kuwekeza kwenye sekta ya utalii.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI